****************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAKAZI katika Vijiji vya kata ya Talawanda , Chalinze ,Bagamoyo Mkoani Pwani, wametakiwa kuchangamkia kilimo cha Miwa watayoiuza kwenye Kampuni ya Bagamoyo Sugar inayozalisha sukari.
Kampuni hiyo inayozalisha bidhaa hiyo kutokea kwenye mashamba yake yaliyopo Kijiji cha Makurunge , pamoja na kumiliki mashamba makubwa yaliyolimwa kwa wingi zao la miwa, lakini bado wanauhitaji mkubwa wa zao hilo.
Diwani wa Kata ya Talawanda Ramadhani Biga Akizungumza na wananchi ,baada ya hafla ya uzinduzi wa upandaji wa mikorosho, kwenye Kijiji cha Magulumatali alieleza, Kampuni hiyo licha ya Kuwa na ardhi kubwa iliyopandwa miwa kwenye kijiji hicho, uongozi huo umekaa na halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo kuelezea uhitaji zaidi wa zao hilo.
“Pamoja na kuzindua upandaji wa zao la korosho, lakini niwaombe wakulima wenzangu pia tuelekeze nguvu zetu katika kupanda miwa, kwani kuna soko kubwa kwenye Kampuni ya Bakhresa pale Makurunge,” alisema Biga.
Aidha diwani huyo pia alieleza halmashauri hiyo imedhamiria kufufua za hilo, na kwamba kuna kampuni ipo Kata ya Mandera inayochakata zao hilo.
Aliwaasa wananchi kuhakikisha wanajikita ili kujikwamua kiuchumi.
“Halmashauri yetu katika kuhakikisha inainua maisha ya wananchi wake imeanzisha kitalu cha zao la Mkonge kipo pale Lugoba, hatua hii inalenga kuwapatia fursa wakazi ya kujiongezea kipato kitachowasaidia kusomesha na kujipatia maendeleo kupitia fursa hizo,” alisema Biga.
Mkazi Seleman DudiPendo na Mwajuma Mohamed walisema kuwa wamepokea kwa faraja taarifa hizo na kwamba watakwenda kuzifanyiakazi ili kujiongezea fursa zaidi za kiuchumi.