Meneja wa Metrojia TBS, Bi.Stella Mrosso (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Metrojia TBS, Bi.Stella Mrosso (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Ubora (TBS) Bi.Magdalena Sedemaki akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
***********************
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), linatarajiwa kupokea cheti cha ithibati ya utoaji huduma za uthibitishaji mifumo ya kimenejimenti kutoka kwa Taasisi ya Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADCAS) Mei 12,2022 jijini Dodoma kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja wa kitengo cha uthibitishaji wa ubora wa mifumo, Bi. Magdalena Sademaki amesema kuwa utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho wa utoaji wa huduma bora na baada ya mchakato TBS imeweza kupewa cheti hicho ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Uwezeshaji, Viwanda na Biashara huku wadau, wateja na mashirika mbalimbali wakitarajia kuwepo
Aidha utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho kuwa TBS inatoa huduma kwa mifumo ya kimataifa na kukidhi matakwa ya nchi mbalimbali.
Amesema kuwa cheti cha ubora wanachotoa TBS kimesaidia taasisi mbalimbali kupata masoko mengi nje ya nchi.
Akizungumza juu ya viwango vya usimamizi wa mifumo ya ISO, Meneja wa Metrolojia Bi.Stella Mrosso amesema kuwa husaidia taasisi za umma na mashirika binafsi kuboresha utendaji kwa kubainisha michakato kufuatwa na kutekelezwa na taasisi hizo ili kufuata malengo yao.