Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter (katikati) aakiwa na wajumbe kutoka NACOPHA katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) na serikali kilichofanyika leo Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza jambo na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Eliasi Kwesi katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akiongoza kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma
………………………………………………
Na. WAF– DODOMA
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe ametoa wito kwa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kutoa elimu katika konga za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ili kuongeza hamasa ya watu hao kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO-19
Dkt. Shekalaghe ametoa rai hiyo leo Jijini Dodoma alipofanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter aliyeambapatana na wajumbe wake ambapo amesema kuwa elimu sahihi ikiwafikia walengwa katika konga zao itasadia kuongeza idadi ya uelewa katika jamii na kuhamasisha watu kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa hiari kwa wingi.
Akizungumza Dkt. Shekalaghe amesema kuwa elimu sahihi ikitolewa wakapata asilimia 90 ya watu 7,000 waliochanja na ikatolewa taarfa sahihi kwa jamii itasaidia kuhamasisha watu wengine ambao awaishi na virusi vya ukimwi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko 19
“Hivyo sisi kama Serikali tutajipanga na kuhakikisha viongozi wa Baraza la NACOPHA tunawapatia elimu sahihi juu ya watu kupata chanjo ili waweze kwenda kuelimisha katika konga zilizopo katika jamii na uelewa juu ya watu kuhiari na kupata chanjo ya UVIKO-19”, Dkt. Shekalaghe
Hata hivyo Dkt. Shekalaghe amesema kuwa wao kama Serikali watahakikisha wanapokea mawazo, ushauri na wapo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na Baraza la NACOPHA ili kulinda afya za watanzania.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa huduma ambazo wamekuwa wakizitoa katika baraza hilo hususani matibabu wanayopatiwa pamoja na huduma nyingine zinazolenga mtu anayeiahi na Virusi vya UKIMWI hapa nchini.
“Kumekua na muamko wa watu waishio na kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO-19 hivyo tunaomba serikali kuongeza nguvu kwenye utoaji wa elimu juu ya watu kupata chanjo ya Uviko 19”, ameeleza Peter
Peter ameongeza kuwa wako tayari kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika barala hilo ili kuweza kufikia malengo tarajiwa.