Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka,akizungumza na baadhi ya waumini wa Dini ya Kikristo wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.
Spika wa Bunge Mstaafu Job Ndugai, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa,akizungumza wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Fatuma Mganga,akizungumza wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remedius Emmanuel ,akizungumza wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.
Kwaya ya Wakinamama wakiimba nyimbo mbalimbali za kusifu wakati wa ibada katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Maiko ‘St. Michael’ Wilayani Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Kongwa Mhe. Job Ndugai (kulia) wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Maiko ‘St. Michael’ Wilayani Kongwa.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Ask. Kanoni (mwenye kofia) akionesha cheti chenye orodha ya majina ya wadau waliochangia kununua gari ambalo litatumika katika shughuli za kanisa kwenye ibada iliyofanyika katika kanisa la St. Michael Wilayani Kongwa.
………………………………
Na Bolgas Odilo-KONGWA
MKUU wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,amewataka viongozi wa dini kutumia nyumba zao za ibada kuelimisha masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo zoezi la sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu.
RC Mtaka ameitoa wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.
“Tunawashukuru viongozi wa dini kwa kutupa ushirikiano katika mambo mbalimbali ikiwemo wakati wa chanjo ya UVIKO-19 na sasa tunapokwenda kweny sensa tunaomba ushirikiano wenu wa kutosha kufanikisha zoezi hili”amesema Mtaka
Aidha amewapongeza waliofanikisha kupatikana kwa gari hiyo ambayo itatumika na kanisa hilo kutatua changamoto za usafiri kila linapo hitajika.
Mtaka,amesema kuwa jambo ambalo limefanywa na waumini hao kununua gari bila kusubiri msaada ni jambo la kuigwa na watu wote.
“Lazima sisi kama waumini tuache kitu ambacho tutaendelea kukumbukwa na kanisa na kuwapa wepesi viongozi wa dini katika mahubiri yetu tukifa siyo kutunga uongoo kwenye maziko yetu”amesema
Aidha amesema kuwa suala la elimu kwa watoto na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili waje kuwa viongozi bora wa baadae.
“Somesheni watoto wenu wapate ujuzi ili waje kuendeleza Wilaya ya Kongwa na atakayekutoa kwenye kina kirefu cha maji ni motto wako.
“Kama mlivyosikia hapa Mbunge wenu Mhe. Ndugai anastaafu mwaka 2025 sasa inabidi tupate mtu atakayemrithi itakuwa jambo la aibu tukikosa wa kumrithi kutokea hapa,” ameongeza Mtaka.
Kwa upande wake Spika wa Bunge Mstaafu Job Ndugai, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa,ameweka wazi dhamira yake ya dhati ya kutaka kustaafu ubunge wa Kongwa pindi ifikapo mwaka 2025.
Ndugai ameeleza kuwa suala la kustaafu mwaka 2025 lilikuwa ni la muda mrefu hivyo hastaafu kwa kushindwa uongozi na wala hastaafu kwa kuwa wananchi wa Kongwa hawamtaki.
“Mwaka 2025 wakati huo ukifika na mimi nitakuwa nastaafu Ubunge wa Kongwa nanyi nyote mnalijua hilo.
“Sistaafu kwa kushindwa na sistaafu kwa kuwa hamnitaki hili jambo nilishalipanga toka kitambo sana na sio la jana wala la juzi cha msingi tuendelee kuombeana,” amesema Mhe. Ndugai.
Awali Askofu wa Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa Jacob Chimeledya, amesema kuwa ni aibu kuendelea kutegemea wahisani katika kila jambo.
“Ni aibu sisi watanzania tulivyo na rasilimali za kutosha kuendelea kusubilia wahisani kutoka nje kufanyia mambo yetu ni aibu pia kiongozi wa serikali kuitangaza Tanzania kuwa ni masiki licha ya uwepo warasilimali za kutosha wazungu ndiyo walituaminisha vibaya kuwa sisi ni masikini lakini ukweli sisi siyo masikini kabisa”amesema Askofu Chimeledya
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Fatma Mganga amewataka wanawake wote wa Mkoa wa Dodoma kushirikiana katika jambo lolote la kimaendeleo ili kuleta matokeo chanya katika jamii.