*************************
NA FARIDA SAID, MOROGORO.
Serikali imeiagiza mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha inaweka progamu maalumu na mikakati madhubuti itakayo wawezesha wananchi hasa wakulima na wajasiliamali wadogo kuingia mikataba ya kisheria ili kuwasaidia kuzalisha mazao ya kutosha na kupata masoko ya uhakika.
Agizo hiloimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji kwenye ufunguzi wa maonyesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
AIDHA Shigela alisema Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji kwa kuzingatia maslahi ya wananchi pamoja na kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ili kuhakikisha malengo yanafikiwa kwa kuwa sekta binafsi zina mchango mkubwa katika uwezeshaji wananchi kwa kutoa mikopo na ujuzi kwa wafanyabiashara.
Ilisema kutokana na kufunguliwa kwa Soko Huru la Bara la Afrika (African Continental Free Trade Area – AfCFTA), amewataka wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kuongeza ubora wa bidhaa ili kumudu ushindani wa soko la ndani na kimataifa.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng’i Issa alisema kwa miaka mingi Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa lengo la kuwaondoa umaskini,ambapo imekuwa ikitoa mikopo yenye mashart nafuu,ruzuku pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi.
Aidha alisema hadi kufika Machi, 2022, mifuko na programu za uwezeshaji zinazotoa mikopo na dhamana yenye thamani ya Shilingi Trioni 5.38 kwa wajasiriamali 8,829,595 wakiwemo wanawake 4,596,602 na wanaume 4,232,993.
Akizungumza katika maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Wakili Msomi Albert Msando amewataka wajasiliamari kutumia vizuri maonyesho hayo katika kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali.