*************
Kwa mujibu wa habari toka kwa mwenyekiti wa chama cha Karate cha Jundokan So Honbu chenye makao yake makuu mjini Naha, Okinawa, Japan master Kancho Yoshihiro Miyazato. Baada ya miaka karibuni mitatu sasa walimu wa karate toka Japan, waliziwiliwa kutoka nje na pia kuingia kwa wageni nchini Japan kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, Covid-19 (UVIKO-19).
Serikari ya Japan, imeamuru kuanzia mwezi Juni, 2022 watu wataruhusiwa kutoka na pia kuitembelea nchi ya Japan, baada yakutoa vikwazo vya safari hizo kwa muda mrefu.
Hii imewapa nafasi wafuasi wa Karate duniani kuanzisha safari zao kutembelea katika chimbuko la Karate duniani, visiwa vya Okinawa.
Hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya chama cha Jundokan, waalimu wa kuu (Masters) Kancho Miyazato, sensei Tetsu Gima, sensei Tsuneo Kinjo, Sensei Kazuya Higa, sensei Takayuki Miyakozawa na sensei Aono wa chama hicho toka mjini Naha, Okinawa, watajumuika na walimu wote wa bara la Ulaya, Marekani na Afrika katika semina ya mafunzo ya kila mwaka (Gasshuku) mjini Enkoping, Sweden yatakayo fanyika tokea tarehe 7 hadi 10 mwezi Julai, 2022 ikiwemo nchi za Tanzania, Afrika ya Kusini na Angola.
Kutokana na maelezo ya mkuu wa tawi la chama hicho cha Jundokan Tanzania (Shibu-Cho) Sensei Fundi Rumadha, alieleza kwamba kutakuwa pia na semina maalum kwa wana Jundokan wote toka miji ya Dar es salaam, Dodoma na Mafinga, Iringa, Tanzania na kufanya mitihani ya ngazi mbalimbali za mikanda mieusi kwa wanafunzi takribani tisa au kumi watakao panda ngazi toka mkanda mweusi hatua ya kwanza yaani “Shodan”, hatua ya pili “Nidan”, nah atua yatatu “Sandan”, digrii ya kwanza hadi ya tatu.
Baada ya kuhitimu ngazi ya daraja la tatu yaani “Sandan:, majina yote na orodha yao huthibitishwa kwa mwenye kiti wa chama hicho Kancho Yoshihiro Miyazato mwenye mamlaka ya kuwafanyia mtihani wa daraja la nne hapo miaka ya baadae kupitia maandalizi maalum ya moja kwa moja toka Okinawa kwa “Zoom” chini ya usimamizi wa sensei Fundi Rumadha.
Wanafunzi wa tarajiwa kupandishwa ngazi watatajwa majina yao baada ya kuhitimu mitiani yao mwezi wa Juni mjini Dar es salaam