WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Moshi Vijijini, Prof.Patrick Ndakidemi (CCM),akichangia hoja wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM) Mhe.Augustino Vuma,akichangia hoja wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe Neema Lugangira,akichangia hoja wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Ubungo (CCM) Prof.Kitila Mkumbo,akitoa ushauri kwa Serikali wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge Viti Maalum anayewakilisha Vyuo Vikuu, Dkt. Tea Ntala,akichangia hoja wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu akiwakilisha kundi la Vijana Mhe Judith Kapinga,akichangia hoja wakati Mkutano wa kupokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia leo Mei 7,2022 bungeni jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imepokea maoni ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mabadiliko ya Mitaala kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakichangia maoni yao wabunge hao leo Mei 7,2022 jijini Dodoma katika Mkutano wa kupokea maoni ya wabunge juu ya maboresho ya sekta ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu ya msingi.
Wabunge hao wameishauri serikali kutumia lugha ya Kiingereza katika kufundishia badala ya kulikimbia tatizo la kutokuwa na walimu wenye uweledi wa kufundisha kwa lugha ya kiingereza, walimu hao wanatakiwa kwenda kunolewa ili wapatikane walimu stahiki.
Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Viti Maalumu, Shari Raymond(CCM) amesema kuwa watoto wa zama hizi hawaijui lugha mama (lugha za makabila) zaidi ya Kiswahili hivyo ni vema wakafundishwa kwa kutumia kiingereza.
“Bado hatujafikia wakati wa sisi kutumia lugha yetu Kiswahili kufundishia masomo, kiingereza kipewe kipaumbele tena kianze kutumika kuanzia darasa la kwanza,”amesema
Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo, Prof.Kitila Mkumbo(CCM) akichangia hoja hiyo, amesema kuwa nchi za Asia kama vile Singapore inatumia kiingereza na kufanikiwa kukua kiuchumi.
Naye Mbunge wa Moshi Vijijini, Prof.Patrick Ndakidemi (CCM) amesema kuwa Tanzania isipotumia kiingereza watanzania watapata tabu kupata ajira nje ya nchi.
“Kuhusu lugha ya kutumia nitakuwa mkweli, mfano tukisema tunakwenda na kiswahili moja kwa moja ilihali hatutajiandaa kuwa na maneno kamilifu ya kiswahili kwenye sayansi, ukitoka hapa na kiswahili chako ukienda Kenya, Uganda au pengine utabaki hapo hapo Tanzania..
“Mawazo yangu kuhusu lugha ni kwamba lugha ya kiingereza inatumika duniani kote, hivyo tuipe kipaumbele la sivyo tutakapotoka hapa kwenda kwa wenzetu tutapigwa goli,” amesema
Ametolea mfano majairani nchini Kenya, akisema kuwa Wakenya wanawazidi Watanzania katika soko la ajira kwa sababu wanajua kiingereza.
Awali, Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,amesema kuwa hadi kufikia Disemba mwaka huu atahakikisha rasimu ya maboresho ya sera na mitaala yake imepatikana wakati kufikia Januari mwaka 2023 wataanza mchakato wa kupata idhini serikalini.
“Tumezungumza na wabunge lakini tutakuwa na Kongamano mwisho wa mwezi huu tutaleta wadau wengi kuendelea kupokea maoni tena, tutapokea maoni mtandaoni na kwenye simu halafu tutakuwa na makundi ya kujadili, pia mwisho wa mwezi wa sita tutakuwa na mkutano mkubwa kimataifa wa elimu utafanyika Dar es salaam, mkutano unahitaji wataalamu zaidi tutakuwa na kubadilishana mawazo na sisi tutatumia fursa hiyo kusikilizia wenzetu wamefanya nini,”amesema.
Prof.Mkenda amesema kuwa dunia hivi sasa ina msukumo mkubwa wa mageuzi ya elimu ambapo kuna mpango wa kusamehe madeni au kupata misaada kwenye nchi zinazofanya mageuzi ya elimu.
“Mageuzi tunayokwenda nayo yatakuwa ni makubwa kwa nchi yetu hatutaki kubahatisha, hatuhitaji kukurupuka ndio maana tunahitaji sana kusikiliza maoni yetu,”amesema.