**********************
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
KIONGIZI wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahir Geraruma, amekemea baadhi ya watendaji na viongozi wanaopuuzia mambo kwenye miradi ya maendeleo kwani kwa kufanya hivyo ,ni kusababisha kuchelewa kwa miradi na kuwaacha wananchi wakiendelea kutaabika.
Pia ameendelea kusisitiza uhifadhi wa nyaraka za miradi kwa Ajili ya kumbukumbu za ukaguzi .
Akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha Afya Pangani, Mji wa Kibaha Mkoani Pwani ,Geraruma, aliwaasa baadhi ya viongozi na watendaji waache kufanya kazi kwa mazoea kwa maslahi ya wananchi.
Akipokea taarifa ya dawa za kulevya -kata ya Mwendapole, Geraruma aliwaasa vijana kuacha kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kwani zinamaliza nguvu kazi ya kundi la vijana.
Aliwataka wachapekazi na kujiingiza katika vikundi mbalimbali vya ujasiliamali kujishughulisha kuliko kupoteza muda kuvuta bangi, ama kutumia madawa ya kulevya ambayo yanaathari kwao kiafya .
Geraruma alitoa Rai kwa wale walio tayari kuacha madawa ya kulevya waache na waanze dawa zitakazowasaidia kuacha kwa kuondoa makali ya wingi wa dawa hizo mwilini (methadone).
Awali akipokea mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji wa Kibaha ukitokea wilaya ya Kisarawe , kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailmoja, Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alisema mwenge huo utatembelea miradi 11 yenye thamani ya sh.Bilioni 1.6.
Alieleza kwamba, kati ya miradi hiyo mradi mmoja utazinduliwa ,miwili itawekwa jiwe la msingi ,miwili itatembelewa ,sita ujumbe wa mwenge itapokelewa na mmoja ambao Ni wa Kukabidhi vifaa vya ujenzi Shule ya Sekondari Sofu, huku ukikimbizwa kwenye umbali wa Km. 68.7.
Miradi hiyo iliyotembelewa na kukaguliwa Ni Pamoja na Mradi wa malaria Kituo cha Afya Mkoani,Ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Bundikani, na Mapambano dhidi ya rushwa – Shule ya Sekondari Bundikani.
Miradi mingine ,Ni barabara ya lami Picha ya Ndege – Lulanzi, Kutembelea kiwanda cha Mtanga Polytechnic – Sofu, Kupokea taarifa za lishe, VVU, Sensa ya Watu na Makazi – viwanja vya Kwa Mbonde,kata ya Picha ya Ndege,Kutembelea Kikundi cha Vijana cha Republic kilichopo Mwendapole.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Mkoani Pwani Mei mosi na sasa upo Halmashauri ya sita wilaya ya Kibaha, ambapo Halmashauri Tisa zitafikiwa kimkoa.