Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze amewaasa wananchi wa Chalinze kuendelea kuliombea Taifa na Serikali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa .
Aliyasema hayo wakati aliposherehekea Sikukuu ya Eid kwa kuswali na wanakijiji wenzake wa Kijiji cha Msoga, na kwenda kuwaona wazee wa mji wa Chalinze.
Aliwataka wananchi pia kuwa na Umoja na kushikamana pasi kusahau kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan afanikishe malengo ya kufikia maendeleo makubwa ya uongozi wa Nchi.