Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) linapenda kumkumbusha kila mwekezaji anayetaka kuanzisha mradi Tanzania bara baada ya kupata ardhi anatakiwa kusajili mradi NEMC kwa ajili ya kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na mradi kuidhinishwa na kupatiwa cheti kabla ya kuanza utekelelezaji wake. Aidha, kwa miradi ambayo imeanza utekelezaji pasipo kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira inatakiwa kusajiliwa kwa ajili ya kufanyiwa Ukaguzi wa Awali wa Mazingira.
Vilevile Mwekezaji anapaswa kuzingatia na kutekeleza masharti yote ya Cheti ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa NEMC ya Ukaguzi kila mwaka.
Hivyo Baraza linawakumbusha wawekezaji kuzingatia matakwa hayo ya Kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa ada na tozo za mwaka kabla ya tarehe 15 Mei mwaka huu wa 2022. Baada ya hapo NEMC itafanya ukaguzi nchi nzima na kuchukua hatua za Kisheria kwa wote ambao watakuwa hawajazingatia matakwa hayo ya Kisheria.
Kwa wale ambao hawaja lipa ada za mwaka wanaweza kupata namba ya udhibiti wa malipo kupitia simu nambari 0677 069967 au tembelea ofisi za NEMC Makao Makuu au Ofisi za Kanda.