MOSI 2022: Wafanyakazi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakipita na bango lao mbele ya mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, kwa maandamano katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakiadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani- Mei Mosi 2022.
Baadhi ya Watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi wakiwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam (leo) wakifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mhe. Amos Makala, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakiwa katika maandamano kwenye sherehe za Mei Mosi, katika Uwanja wa Mka Uhuru mkoani Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Amos Makala. Mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Idrissa Shakiru ambaye ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa TANESCO, Bi. Judith Gowele akitoa nasaha zake katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu Mei Mosi..
Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za TGDC Msasani jijini Dar es Salaam
Mfanyakazi bora wa TGDC kwa mwaka huu, Bi. Cynthia Kuringe akitoa neno na kuelezea jinsi tuzo hiyo itakavyozidi kuimarisha ari katika utendaji wake wa kazi kila siku Ariph Kimani akitoa nneo la shukrani katika hafla ya wafanyakazi wa TGDC iliyofanyika katika ofisi za TGDC Msasani jijini Dar es Salaam
**********************************
Wito umetolewa kwa watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) kuendeleza umoja na mshikamano ili lengo kusudiwa la kuzalisha megawati 60 zinazotokana na Jotoardhi kufikiwa kitu ambacho kitachochea ukuaji wa uchumi nchini.
Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Idrissa Shakiru katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za TGDC Msasani jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa ikilinganishwa na waliotoka kwa sasa TGDC iko karibu kufikia malengo yake.
Mhandisi Shakiru ameendelea kwa kusema kuwa, misingi mikuu ya mafanikio katika utumishi wa umma ni pamoja na kujituma, kuwa na nidhamu na kufanya kazi kama timu.
“Utumishi wa umma ni safari ndefu hadi kufikia kustaafu, ili tuweze kufika huko na kupata mafanikio, tunapaswa kujituma, kuwa na nidhamu na kufanya kazi kama timu, kwa umoja na mshikamano” alisema Mhandisi Shakiru ma kuongeza
“Pia mtumishi wa umma unapaswa kuwa committed na uhakika pale unapotegemewa kutimiza majukumu yako basi tija ionekane na uweze pia kujiongoza mwenyewe bila kusubiri kusukumwa”
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, Meneja Rasilimaliwatu na Utawala wa TANESCO, Bi. Judith Gowele amewaasa watumishi hao wa TGDC kuzingatia nidhamu wawapo kazini na katika majukumu yao kwani nidhamu ni moja ya sababu ya kuweza kumfikisha mtumishi katika kilele cha mafanikio.
BI. Gowele ameongeza kuwa, ushirikiano uliopo ni muhimu kuendelezwa na kuomarishwa ili kuweza kufikia malengo ya kampuni ambayo kupitia watumishi ndio nyenzo pekee ya kufikisha malengo hayo.
Katika hafla hiyo, Bi. Cynthia Kuringe ametangazwa kuwa mfanyakazi bora wa TGDC kwa mwaka huu ambapo amezawadiwa luninga.
Akiongea mara baada ya kutangazwa, Bi. Cynthia amesema, amepokea kwa furaha tuzo hiyo na kusema kuwa itamuongezea motisha ya yeye kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuongeza kuwa, watumishi wote katika kampuni hiyo ni bora lakini yeye amekuwa ni mwakilishi wao kwa mwaka huu.
Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, Ariph Kimani amepongeza jitihada za kufanyika hafla hiyo ambapo amesema pamoja na mambo mengine inasaidia kuimarisha mahusiano mema kazini, mapenzi baina ya wafanyakazi na ufanyaji kazi wa pamoja kama timu kuelekea kutimiza malengo waliyojiwekea.
Awali, watumishi hao kutoka TGDC walishiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kwa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kimkoa yamefanyika katika uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.
Siku ya Wafanyakazi huadhimishwa kila mwaka ikiwa na lengo la kutambua na kuenzi mchango wa Wafanyakazi katika maendeleo ya mataifa mbalimbali na kwa Tanzania, kitaifa siku hii imeadhimishwa katika Mkoa wa Dodoma huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa ni mgeni rasmi.
Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema ‘MISHAHARA NA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NDIO KILIO CHETU, KAZI IENDELEE’