Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mohamed Mtanda akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Prof. Hubert Gijzenz akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Deodatus Balile, akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.Mkurugenzi wa Mawasilianon wa Tume ya Muungano wa Umoja wa Afrika, Musabayana Wynne Zvinaiye akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Balozi Manfredo Fanti, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania mara baada ya ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi ( wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wakipitia mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali kabla ya ufunguzi wa maonesho hayo kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
***************************
Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amewataka wanatasnia ya habari barani Afrika kuhakikisha wanaisaidia jamii kubadili mtazamo kwa kuona fursa zilizopo na kujivunia kuwa sehemu ya bara la Afrika lenye rasilimali za kutosha
Waziri Nape amezungumza hayo akizindua maonesho ya utangulizi kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika Mei 3 ya kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu wa 2022 Tanzania imekuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kwa Bara la Afrika yanayofanyika katika jijini Arusha
“Bara letu la Afrika lina rasilimali nyingi za kutosha na maeneo mengi rasilimali hizi zimegeuka kuwa laana kwa watu nadhani wakati umefika kwa wanahabari tuchukue uamuzi wa kusaidia bara letu lifaidike na rasilimali zake na watu wake waone matokeo ya baraka za rasilimali kwenye jamii zetu,”
Ameongeza kuwa, “Inauma kuona tunateswa na rasilimali zetu wenyewe kwa sababu tunaona maeneo yenye rasilimali za kutosha ndio kwenye magomvi mengi na ndipo ambapo watu wake wanateseka sana lakini ukipewa hesabu ya rasilimali tulizonazo ukilinganisha na mabara mengine hatupaswi kuwa hapa tulipo hivyo wanahabari tusimame kubadilisha mtazamo wa mambo haya na ninaamini inawezekana kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake.”
Katika hatua nyingine Waziri huyo amezungumzia changamoto za tasnia ya habari zinazotokana na mabadiliko ya kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuwa hazikwepeki na hata tukiamua kusubiri bado mabadiliko hayo duniani yatatulazimu kwenda katika ulimwengu wa dijiti
Aidha, amesema kwa upande wa Serikali ya Tanzania, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndilo lenye dhamana ya kutunga, kurekebisha au kufuta Sheria ambazo zinakuwa hazitekelezeki au zinazokinzana na hali halisi hivyo Wizara anayoiongoza inaendelea kukamilisha uwasilishaji wa mapendekezo ya marekebisho ya sheria tajwa kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za uwasilishaji wa mapendekezo hayo na Bunge lipo tayari kupitisha
Amesema kuwa mabadiliko ya kidijiti yamechangia kutokea kwa mijadala mikubwa inayoendelea kuhusu crypto currency na usalama wa mifumo ya kielektroniki hivyo amewataka wanahabari kutumia taaluma zao kufanya uchambuzi na kuainisha fursa zinazokuja na maendeleo ya kidijiti ili kusaidia jamii zetu kuziona fursa kwenye mabadiliko hayo
“Tumepewa kalamu na uwezo wa kusaidia jamii zetu na kila mmoja akiamua kutekeleza wajibu wake hili linawezekana”, Amezungumza Waziri huyo
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Wizara inaendelea kusimamia, kuboresha na kuwezesha upatikanaji wa fursa zinazotokana na mabadiliko ya kidijiti na kuifanya Wizara hiyo kuwa Wizara muhimu inayosimamia Sekta muhimu zinazochangia uchumi wa nchi na Wizara itaendelea kushirikiana na wanahabari kuboresha mazingira ya kufanya kazi kwa uhuru, ubunifu na kwa mujibu wa sheria
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka huu wa 2022 yana kauli mbiu ya “Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti” kwa Bara la Afrika yanafanyika jijini Arusha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari