Na Fredy Mgunda,Iringa
MKUU wa mkoa wa Iringa amepiga
marufuku kwa wafanyabiashara kupandisha bei kiholela kwa ajili ya kupata faida
hivyo wanatakiwa kupandisha bei kwa kufuata sheria za nchi ili kuondolea
maumivu wananchi wa kawaida ambao ndio wanunuaji wa bidhaa hizo.
Akizungumza mara baada ya
kufanya ziara ya kuangalia kuagalia namna gani bidhaa zilivyopanda bei mkoani
Iringa,Mkuu wa mkoa Queen Sendiga alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara
wamekuwa wanatumia kigezo cha kupanda bei kwa mafuta nao ndio wanapandisha bei.
Sendiga alisema kuwa
wafanyabiashara wakipandisha bei kiholela wanawaumiza wanunuzi na wananchi wa
kipato cha nchi hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kupandisha bei kwa kufuata
sheria na tamko rasmi kutoka serikalini.
Akiwa katika ziara hiyo mkuu wa
mkoa wa Iringa alibaini kuwa vituo vyote vya mafuta ya Petroli na Dizel vinauza
mafuta hayo kwa kufuata sheria za nchi na muongozi ulitolewa na mamlaka husika
hivyo aliwapongeza wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta.
Sendiga alisema kuwa
wafanyabisha wengi wamepandisha bei kwenye vyakula,matunda na bidhaa nyingine
ambazo zinazalishwa kwenye viwanda ambavyo vipo nje ya mkoa wa Iringa jambo
ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi kwa mamlaka nyingine zinazohusika.
Alisema kuwa ikibaini kuna mfanyabisha
amepandisha bei kiholela atachukuliwa hatua kali za kisheria na hakutakuwa na
msamaa kwa mfanyabiashara huyo.
Sendiga alizitaka mamlaka ya
udhibiti usafiri ardhini (LATRA) na wakala wa vipimo (WMA) kufanya kazi
zao kwa weredi kwa kuwa wameoneka kuwa wameshindwa kudhibiti vipimo vya mizani pamoja na baadhi ya mabasi
kupandisha bei nauli kinyume na sheria.
Kwa upande wa baadhi ya
wafanyabishara wa mkoa wa Iringa walisema kuwa kupanda kwa bei ya mafuta ya
magari kumesababisha kupanda kwa gharama za usafirishaji na uzalishaji wa
bidhaa za viwandani hivyo kusababisha nao kupandisha bei.
Walisema kuwa wanalazimika
kupandisha bei za bidhaa mbalimbali ambapo inaonekana kama mzigo wote huo
unamuangukia mtumiaji wa mwisho wa bidhaa hizo.
Aidha wafanyabiashara hao
walimuomba mkuu wa mkoa wa Iringa kufikisha kilio chao kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan juu ya mfumko wa bei ambao
unaendelea maeneo yote nchini.