WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda ,akisikiliza taarifa ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma ikisomwa na Mshauri mwelekezi wa mradi huo Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akipata maelezo ya ramani ya Chuo cha Ufundi Dodoma muonekano wake kitakapokamilika kutoka kwa Mshauri mwelekezi wa mradi huo Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akiendelea na ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akitoa maelekezo kwa Mshauri mwelekezi wa mradi huo Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Noel Mbonde,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akipata maelezo kutoka kwa Mshauri mwelekezi wa mradi huo Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
MAFUNDI wakiendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo May 2,2022 mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma .
MKURUGENZI wa Elimu ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Noel Mbonde,akizungumza na waandishi wa habari baada ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,jijini Dodoma leo May 2,2022.
………………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa kuna mageuzi makubwa ya mitaala yanakuja nchini ambayo wanaifanyia mapitio ya sera ya Elimu ya mafunzo ya mwaka 2014.
Hayo ameyasema leo Mei 2,2022 jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kilichopo Nala,Prof.Mkenda amesema kwa sasa wanakuja na mabadiliko makubwa katika mitaala na sera lengo likiwa na kuongeza ubora wa elimu hapa nchini.
“Kazi hii ya kupitia sera na kubadilisha mitaala inafanyika na naamini kwa kazi tunavyooenda sasa hivi mwezi Desemba tutakuwa na rasimu ambayo itakuwa inasubiri maamuzi ya Serikali na kutakuwa na mageuzi makubwa hapa nchini ya elimu tangu 1967
“Lakini mageuzi hayo yatahitaji miundombinu mitaji na vifaa kwahiyo chuo kama hiki ni sehemu muhimu ya kutupeleka katika mageuzi hayo.
“Maoni tumeishakusanya mwaka mzima na kutakuwa na kongamano la siku tatu tutataka tusikie maoni lakini yameishasemwa ni lazima watu wajue.Tutawaeleza Wabunge ili mwaka huu kazi ya kukusanya maoni tumalize tukifika Desemba tumalize tuwe na rasimu.
“Tunaingia katika maamuzi na ikiishaingia katika maamuzi utekelezaji uanze mapema kabla ya uchaguzi wa 2025.Matarajio ni kwamba tuanze 2026 lakini naamini kwa jinsi ambayo tumejipanga tunaweza tukaanza utekelezaji 2024 angalau kwa awamu kwakweli yajayo katika elimu naamini yanafurahisha,”amesema
Kuhusiana na ujenzi wa Chuo hicho,Waziri Mkenda amesema: “Tunatarajia utakamilika Desemba mwaka huu tumeelekezana kazi ya kutafuta wakufunzi na vifaa ianze kuna Mradi wa Benki ya Dunia tutapata fedha.
“Itakuwa ni 2023 tutakuwa tumepata vifaa na wakufunzi tutakuwa na wataalamu kutoka nje waje na wa kwetu waende kule na Wataalamu kutoka Uturuki waje maana kila mtu anataka suti ya Uturuki lazima tujifunze kwa wenzetu,”amesema.
Amesema Chuo hicho ni kikubwa na kitakuwa ni cha nne na kitakapokamilika kitachukua wanafunzi 3000 ambapo kwa awamu hii kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1500 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 17.9 zitatumika.
“Kama mnavyofahamu hapa nchini tuna vyuo vya Veta 43 vya Serikali lakini kwa msukumo mkubwa tunatarajia mwisho wa mwaka huu tunaweza kuwa na vyuo 77 ambavyo vinafanya kazi
“Ujenzi wa majengo mapya tuna vyuo 25 vya Wilaya vinajengwa vinne vya Mikoa na kuna vingine vimejengwa na Halmashauri tukichukua hivyo 43 tukichanaganya vitakuwa 77 kazi itakuwa ni kuweka vifaa na kupata wakufunzi.
“Kwa ujumla vyuo vya ufundi vya Serikali na binafsi ni 881 sasa tunaelewa mageuzi makubwa ya mitaala yanakuja tunafanya mapitio ya Sera ya elimu ya mwaka 2014 na maelekeo ya Rais tutakapokamilisha tuhakikishe tunaongeza mambo ya ufundi ili wanamaliza waweze kuajirika,”amesema.
Amesema wanataka kutengeneza Veta katika kila Wilaya na mazungumzo yameishaanza na watapata Mkopo kutoka Benk ya Dunia.
“Sitarajii ujenzi huu uwe chini matarajio yangu ni makubwa sana kazi kubwa ni kuhakikisha maji na umeme unafika.Ujenzi ukikamilika tutamuomba Rais aje auzindue huu mradi kwahiyo kuendeleza elimu ya ufundi ni pamoja na kufundisha walimu,”amesema.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Noel Mbonde amesema fani tatu zitaanza kufundishwa katika Chuo hicho ambazo ni nishati,afya na ujenzi.
“Kwa awamu hii ambayo tumeanza nayo vikikamilika tutaongeza idadi ya vijana wenye ujuzi kwa zaidi ya asilimia 30,”alisema.
Amesema kwa wastani kwa mwaka katika Vyuo vya Ufundi na ufundi wa kati zaidi ya wahitimu 150,000 huwa wanahitimu.
Awali akitoa taarifa ya Mshauri Mwelekezi wa mradi huo Bw.Aliki Nziku,amessma kuwa utekelezaji wa (DTC), upo katika awamu ya kwanza inayojumisha ujenzi wa jengo la utawala,bwalo la chakula, majengo mawili ya vitivo ( Departmental buildings), majengo ya madarasa yenye vyumba sita, karakana tatu za mafunzo kwa vitendo.
Bw.Nziku amefafanua kuwa pia ujenzi huo umejumuisha mabweni mawili ya gorofa tatu Kila moja lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 300, nyumba za Watumishi nne na Zahanati.
“Awamu hii ya kwanza ikikamilika itachukua wanafunazi 1500 na mradi mzima utakapo kamilika utachukua wanafunzi 3000,” amesema Mhandisi Nziku.
Mshauri huyo amesema kuwa mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi CRJ (EA), LTD kwa gharama ya shilingi bilioni 17.9 na kwamba kwa niaba ya wizara hiyo mradi unasimamiwa na washauri waandamizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Bureau of Industrial Cooperation (BICO), wakishirikiana na washauri waandamizi kutoka Arqes Africa na Build Consul.
“Tuna Wizara kuendelea kutupatia ushirikiano zaidi ili kukamilisha mradi wetu kwa wakati kama ulivyokusudiwa pia tinaomba hatua zaidi kufuatilia suala la umeme na maji kufika kwenye mradi kwa wakati,” amesema.