Afisa wa uhamiaji Mkoa wa Mwanza Peter Mbaki akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa ya kukamatwa wahamiaji haramu
Afisa wa uhamiaji Mkoa wa Mwanza Peter Mbaki akizungumza na kuwaonyesha wahamiaji haramu waliokaa chini
*************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Idara yauhamiaji imetoa anagalizo kwa baadhi ya wananchi wanaoshiriki kufanya makosa ya uhamiaji kwa maana ya kusaidia kuwasafirisha,kuwahifadhi wahamiaji haramu.
Angalizo hilo limetolewa leo hii Mei 2,2022 na Afisa uhamiaji Mkoa wa Mwanza Peter Mbaki, wakati akitoa taarifa ya kukamatwa wahamiaji haramu 68 raia wa Ethiopia.
Mbaki amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995 sura namba 54 ukikamatwa kwa makosa ya usafirishaji unaweza kuhukumiwa kifungu cha miaka 20 jera au faini ya milioni 20.
Mbaki amesema kuwa Aprili 4,2022 idara hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la polisi walifanikiwa kuwakamata wahamiaji hao wenye umri kati ya (14-25) katika Kijiji cha Sanjo Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi.
Amesema kuwa madhumuni yao walikuwa wanataka kwenda Afrika Kusini na walikuwa wamehifadhiwa na raia wa Tanzania Tarika Alex(26) ambae pia amekamatwa akiwa kwenye nyumba ya mtu aliefahamika kwa jina moja la Joseph.
Mwisho Mbaki ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini,kuwakamata na kuwachukulia hatua wahamiaji haramu na wahalifu wote.