*******************
Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Sahir Geraruma ,ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya 830KJ Kibiti ,Mkoani Pwani,ambao umekamilka kwa asilimia 100 na uko tayari kutoa huduma ndani ya jamii inayoizunguka.
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia ufadhiliwa na Shirika la global A Network linalotoa msaada wa kuchimba visima virefu Kibiti, kwa kushirikiana na Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) wameweza kutekeleza mradi huo pamoja na visima vingine 19 vyenye thamani ya sh. milioni 380 wilayani hapo.
Akizindua mradi huo kata ya Mchukwi,Mkupuka mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru wilayani Kibiti ukitokea Rufiji, Geraruma alisema mradi umekidhi vigezo .
Alielekeza Tanki la kisima linafaa kulindwa ,kuhifadhiwa na kuimarisha ulinzi ilihali kujiepusha na lolote ambalo linaweza kuleta madhara kwa watumiaji.
Pia alitembelea mradi wa shamba la kilimo Cha korosho na ufuta lenye ukubwa wa hekari 70 .
Vilevile Geraruma, alihimiza mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU,malaria na matumizi ya madawa ya kulevya.
Akielezea juu ya shamba Hilo ,kaimu Kamanda wa 830KJ Kibiti, Meja Victor Nkya alisema kuwa, mradi huo ni endelevu kama inavyofahamika JKT imejikita kwenye shughuli za kilimo ili kutoa elimu kwa vijana wa jeshi wanaopata mafunzo kwa mkataba wa miaka miwili na wa mujibu wa sheria.
Meja Nkya alifafanua, Lengo ni kuendelea kujengea uwezo kikosi kwa ajili ya kuinua mapato.
Awali akisoma taarifa ya mradi, Kapt.Yusuph Matias Masalu wa 830KJ Kibiti , alisema kikosi kilianza jengo la muda la Zahanati Lakini baadae makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kutumia fedha za maendeleo ya mwaka wa fedha za maendeleo ya mwaka wa fedha 2020-2021.
“Ikakijengea kikosi Zahanati yenye jengo la kudumu ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 99 Lakini bado hakukuwa na huduma ya maji”
“Serikali inayoongozwa na Rais Samia kupitia Shirika Hilo la Grobal kwa kushirikiana na RUWASA wameweza kuchimba visima 19 Kibiti kwa milioni 380 “alisema Masalu.
Masalu alibainisha, wafadhili hao na RUWASA walifanya utafiti wa maji chini ya ardhi na kuchimba kisima hicho ,chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 11,300 kwa saa na urefu wa mita 93 kilichogharimu milioni 20 .
Alieleza, kikosi hicho kimetumia milioni 15.1 Kwa Ajili ya kupima wingi,ubora wa maji, kujenga mnara, kununua tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 10,000, kununua na kufunga pampu kwa Lengo la kutoa huduma ya maji.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti, kanal Ahmed Abbas alisema mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani humo utapitia miradi 15 yenye thamani ya sh.milioni 809.3 na kukimbizwa km.110 kwenye kata tano.
Miradi mingine iliyopitiwa Ni Pamoja na ujenzi wa vivuko vitatu kwenye bonde la Nyarwanza, ujenzi wa madarasa matatu kwa fedha za Uviko19 na mradi wa madarasa matatu kwa fedha za mapato ya ndani Sekondari Mtawanya na mradi wa kituo cha afya Mjawa.
Mwenge wa Uhuru Mei 3 mwaka huu ,unatarajiwa kupokelewa wilaya ya Mkuranga.