Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lulu Mengele (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Lucy Seleko kutoka Wizara hiyo na Mchumi Adeventina Kato Mei 02, 2022.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii- NSSF, Lulu Mengele (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha Mei 02, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiagana na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii -NSSF, Lulu Mengele (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Lucy Seleko kutoka Wizara hiyo na Mchumi Adeventino Kato Mei 02, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii -NSSF, Lulu Mengele (wa pili kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha. Wengine ni Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Mei 02, 2022.
**********************
Na WMJJWM- Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na kuzungumza na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii -NSSF, Lulu Mengele.
Katika kikao hicho Dkt. Zainab Chaula na Meneja huyo wamejadiliana mambo kadhaa ikiwepo utoaji wa elimu kwa kundi la Wamachinga kuweza kujiwekea akiba katika mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF ili iweze kuwasaidia pale wanapozeeka na kutokuwa na uwezo wa kuendelea kufanya biashara zao.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inaweka mikakati na Mipango ya kuwahudumia wananchi.