********
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinachofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika suala la maslahi ya wafanyakazi ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwani ilishaahidi kuweka mazingira rafiki kwa wafanyakazi na kuboresha mishahara.
Pia, CCM imelipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais Samia
kuhusu nyongeza ya mshahara na kulipwa stahiki kwa wafanyakazi waliyokutwa na vyeti bandia.
Aidha, imesema taarifa ya TUCTA ni mwafaka kwa wanasiasa wasio na maslahi na wafanyakazi wala nchi ambao wanaumizwa
na mazuri yanayofanywa na Rai Samia, huku wakiwa wanabadili mazuri kuwa mabaya kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa
kisiasa.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka,ilisema
CCM, kupitia ilani yake ibara ya 130 iliahidi kuwa serikali itakazoiunda itaweka mazingira rafiki ya utendaji wa vyama vya
wafanyakazi ili iendelee kuwa nguzo muhimu katika kujenga mahusiano mahala pa kazi.
“Anachokifanya Rais Samia Suluhu Hassan sioporojo au utashi wake bali ni utekelezaji wailani, Chama Cha Mapinduzi kinampongezasana kwa umakini wake katika kuitekeleza ilanikwa vitendo.
“Katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kupitia ilaniyake ya uchaguzi ibara ya 130 kuwa serikaliitakazoziunda zitaendelea kuweka mazingirarafiki ya utendaji wa vyama vya wafanyakazi iliviendelee kuwa nguzo muhimu katika kujengamahusiano mahala pa kazi na kuboreshamasilahi”alisema