Naibu Afisa Makazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNIFPA) Dkt.Wilfred Ochan akizungumza katika Mkutano wa vijana ulioratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Aprili 30,2022 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Program wa Asasi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNA) Bw.Lucas Kifyasi akizungumza katika Mkutano wa vijana ulioratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Aprili 30,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituoo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamdauni Bw.Emmanuel Lugomela akizungumza katika Mkutano wa vijana ulioratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Aprili 30,2022 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Bi.Hortencia Nuhu akizungumza katika Mkutano wa vijana ulioratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Aprili 30,2022 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa vijana ulioratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Aprili 30,2022 Jijini Dar es Salaam
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Vijana kutoka katika Vyuo mbalimbali nchini wametakiwa kuzitumia changamoto zinazojitokesha katika maisha yao kuwa fursa katika kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha takriba vijana 568 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini ambao umeratibiwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA Tanzania na Makumbusho ya Taifa ikiwa ni katika kuelekea kwenye mkutano wa TIMUN unaotarajiwa kufanyika mwezi huu Mkoani morogoro.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa –YUNA Tanzania Hortencia Nuhu amesema lengo ni kuwawezesha vijana kujadili kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya Afya,mahusiano,kukuza uchumi na kutetea haki za vijana hasa katika elimu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Emmanuel Lugomela pamoja Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Tanzania Anamey Bagenyi wametoa ujumbe kwa vijana hao kuwa wazalendo katika kuendelea kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria.
Lilian Methiw ni mmoja ya vijana kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akiwa ameshiriki katika mkutano huo ameishauri serikali kuandaa matamasha ya mara kwa mara kwa vijana ili waweze kubadilika na kukomesha ukatili wa kijinsia.