NA FARIDA MANGUBE MOROGORO.
Kituo Cha Uwekezaji Nchini ( TIC ) kimejipanga kutatua changamoto za wawekezaji kwa kuwafikia moja kwa moja kwenye maeneo yao ya uzarishaji ili waweze kukua zaidi kiuchumi.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha Mchele mkoani Morogoro iliyo jumuisha wakuu wa Taasisi zinazo simamia sekta ya uwekezaji hapa nchini yenye lengo la kuboresha huduma kwa wawekezaji Mkurugenzi huduma kwa wawekezaji John Mnali alisema Serikali ya rais Samia Suruhu Hassani imejipanga katika kuwakaribisha wawekeza katika sekta mbalimbali.
“Serikali ya Rais Samia Suruhu Hassani imejipanga katika kuwakaribisha wawekeza katika sekta mbalimbali hivyo sisi kama kituo cha uwekezaji tunajukumu la kuhakikisha uwekezaji unaimarishwa katika Nyanja zote kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wageni na wazao.” Alisema Mkurugenzi huduma kwa wawekezaji John Mnali.
Aidha aliesema ushirikiano uliopo kati ya TIC na taasisi nyingine za Serikali utasaidia kutatua changamoto zilizopo sasa ambapo serikali ipo katika mchakato wa kufungua dirisha moja litakalo kutanisha taasisi zote zinazo husika na kutoa vibalikwa wawekezaji kutoka nje zitaunganishwa pamoja.
“Sisi kama kituo cha uwekezaji tunatia juhudi zaidi ili kuona kama kunachangamoto yeyote itakayojitokeza tuweze kuzitatua kwa wakati hivyo niwatoe hofu wawekezaji serikali ipo tayari kuwahudumia.”Alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Meneja wa utafiti kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini TRA Bi.Saada Alluy ambaye alimuakirisha kamishna wa TRA nchini alisema mamlaka hiyo imejiimarisha katika kuhakikisha kila muwekezaji anachangia pato la Taifa bila ya dhumla yeyote.
“Pia naomba nitoe wito kwa wawekezaji wote nchini kama kuna mtu anahisi anatengenezewa mazingira ya rushwa basi atoe taarifa mara moja kwa kamishna wa TRA na TAKUKURU ili hatua za kishria zichukuliwe kwa wahusika au muhusika.”Alisema Bi. Saada
Nae Meneja Rasilimali watu Bwana Deusdeti Kikuna kutoka kiwanda cha kuchakata Mchele mkoani hapa amsema mpaka sasa kiwanda kimetoa fursa za ajira rasmi na sizokuwa rasmi kwa watanzania wengi hasa wakulima wa mpunga pamoja na wanaofanya shughuri za usafilishaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
.