Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu alipojumuika nao katika futari aliyoiandaa jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwakaribisha wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Mama Napono na Nakiteto kushiriki nae kwenye futari aliyoiandaa. Nyuma yake ni Naibu Waziri wa Ofisi yake Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi.
Wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu wakiwasili Serena Hoteli, jijini Dar es Salaam, kushiriki futari iliyoandaliwa na Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwakaribisha wake wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Zakia na Asha kushiriki nao kwenye futari aliyoiandaa kwa wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa salamu kwa wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kwa wake wa viongozi hao wastaafu jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Ofisi yake Mhe. Deogratius Ndejembi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu alipojumuika nao kwenye futari aliyoiandaa jijini Dar es salaam.