Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE
MASEJO amewaambia wananchi Kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji la
Arusha na Mkoa ni shwari kuelekea uzinduzi wa filam ya The Royal Tour.
Kamanda Masejo amesema kuwa Kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya The
Royal Tour Tanzania Kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo limejianga vyema
kuhakikisha dunia inashuhudia uzinguzi huo wa filamu ya the Royal Tour itakayo
fanyika siku ya kesho 28.04.2022 katika kituo Cha kimataifa Cha Mikutano Arusha
AICC.
Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa
wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionyesha dunia ukarimu huo na kuionyesha
dunia kuwa Arusha ni kitovu Cha utalii.