Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Dk. Said Kudra, akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa ujumbe wa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ulipotembelea banda la Barrick kwenye maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra,akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa Wananchi na wadau waliotembelea banda la maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra,akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa Wananchi na wadau waliotembelea banda la maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra,akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa Wananchi na wadau waliotembelea banda la maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akiongea baada ya kutembelea banda la Maonesho la Barrick Bulyanhulu (Katikati) ni Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk. Said Kudra na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Adelhelm Meru
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ,alipotembelea banda la maonesho la Barrick jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Adelhelm Meru, kushoto ni Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Ridhiwan Kikwete (mwenye suti nyeusi katikati) ,alipotembelea banda la maonesho la Barrick jijini Dodoma
*
Serikali imepongeza kazi kubwa na mzuri inayofanywa na mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya uchimbaji wa madini chini ya ardhi bila kulazimisha kushuka chini kama inavyofanyika katika shughuli za uchimbaji katika migodi mingine nchini.
Teknolojia hii imevutia viongozi mbalimbali,Wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya madini wanaoendelea kutembelea banda la Bulyanhulu lililopo Maonesho ya Wiki ya Usalama Mahali pa Kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetin Center jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, alitoa pongezi kwa Barrick Bulyanhulu kwa mgodi wa kwanza nchini kuwa na mitambo ya kieletronikali ya kimataifa katika shughuli za uchimbaji wa madini sambamba na maabara ya kwanza ya kisasa ya kupima madini (Auto-Mining and crysos Photon Assay Laboratory).
Alisema Barrick Bulyanhulu, imefanya mapinduzi makubwa sana ya kidigitali ambayo yanawezesha shughuli za uchimbaji madini kuwa salama tofauti na uchimbaji usio wa matumizi ya teknolojia za kisasa.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Mstaafu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Adelhelm Meru, alipongeza mapinduzi hayo ya kiteknolojia ya Barrick Bulyanhulu, ambayo yamewezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye migodi inayoendeshwa kwa teknolojia na mifumo ya kimataifa ya uchimbaji madini.
Wadau mbalimbali na Wananchi wanaotembelea banda hilo pia wamevutiwa na shughuli za kampuni kuhusu uzingatiaji wa masuala ya Afya na Usalama katika maeneo ya kazi kwenye Mgodi huo.