wWALENGWA wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf wilayani sikonge wakisubiri zamu zao kupokea fedha za mfuko huo
…………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Walengwa wa mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF katika kijiji cha Kipanga Mlimani kata ya Chabutwa wilayani Sikonge mkoani Tabora , wameiomba halmashauri wilaya hiyo kupelekea maafisa mifugo kwa ajili ya kutoa elimu ya ufugaji Kuku ,Mbuzi na Ng’ombe na kutambua matumizi sahihi ya chanjo mbalimbali za mifugo .
Mifugo mingi imekuwa kishambuliwa na magonjwa mbalimbali na wananchi wajui matumizi sahihi ya dawa zinazoweze kuponyesha mifugo yao jambo ambalo wamekuwa kutumia dawa za asili ambazo hazisaidia kuponya magonjwa ambayo yamekuwa yakishambulia Kuku,Bata ,Mbuzi na Ng’ombe
Kauli hiyo ilitolewa na walengwa na kunusuru kaya masikini Tasaf katika kijiji cha Kipanga Mlimani kata ya Chabutwa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora.
Walengwa wa mfuko huo Zafarani Hussein ,Salima Nassib na Pili Mgalula wakizungumzia kwa nyakati tofauti walisema kwamba magonjwa ya mifugo yamewatia umasiki na kuwarudisha nyuma kimaendeleo .
Zafarani Hussein alisema kwamba alikuwa na kuku wa kubwa 200 na kuku wadogo 150 ambao walipata maradhi ya kideli na kufa wote jambo ambalo lilimrudisha nyuma kiuchumi.
Alisema kwamba baada ya kuona kuku wake wakitoa kinyesi cheupe na kijani alitafuta dawa na kuwapatia lakini kila akiwapa dawa hiyo ndivyo vifo vilivyoongezeka siku hadi siku na kufanya kuku wote 350 kufa na kutoambuli kitu chochote.
Nao walengwa wa mfuko huo ambao ni Salima Nassib na Pili Mgalula walisema kwamba maradhi ya kuku yamekuwa janga kubwa kwao kwani wamerudishwa nyuma kimaendeleo kwani walitengeme kuwa na kuku wakubwa 600 kwa kila moja alikuwa na kuku 300 .
“Tulikuwa na lengo la kujiimarisha kiuchumi kwa kuunza kuku ili tuweze kununua Ng’ombe lakini magonjwa ya kuku yameturudisha nyuma kimaendeleo jambo ambalo linatuumiza vichwa kwa sasa tumeanza tena kufunga na tayari tumeanza na kuku 20 ambao tunaomba kupatiwa elimu ya ufugaji na matumizi sahihi ya dawa hizo ilikuweza kujiongezea kipato na niondokane na umaskini’’walisema kina mama hao
Naye mtendaji wa kijiji cha kipanga mlimani kata ya Chabutwa ,Johari Edson alisema kwamba wamekuwa wakiwatumia mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuwelezea wananchi umuhimu ya kuchanja mifugo yao ili kuwaepuka na maradhi yanayoweze kujitokea
Hata hivyo afisa mifugo na uvuvi wa wilaya ya sikonge Dkt Elisha Majebele alisema kwamba wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kuepukana na magonjwa ambayo yanaambukiza kwa njia ya hewa.
Alisema kwamba wananchi wengi wanashindwa kusafisha mabanda yao hivyo kinyesi kikitoka ni rahisi kuambukizana magonjwa ila elimu ya mara mara inafanyika kwa walengwa wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf wilayani Sikonge.
“Tumekuwa tukitoa ushauri kwa wafugaji wa kuku na bata kuhakikisha kila mara wanasafisha mabanda yao yawe masafi ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya hewa”alisema Dkt Majebele.
Magonjwa hatari kwa kuku ni Kipindupindu cha kuku,Ndui,,Kideli,Mdondo,Gumboro ,Minyoo ,Homa ya Matumbo ,Uharo Damu na Mafua makali