***********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa pole na salamu za rambirambi kwa Kanisa Katoriki jimbo la Njombe na serikali ya Mkoa huo kwa kuondokewa na vijana 9 wa umoja wa vijana wa kanisa hilo UVIKANJO ambao walipata ajali ya gari april 24 katika eneo la Igima na kuacha 18 katika tukio hilo.
Vijana wa UVIKANJO walipata ajali wakati wakitoka kuona watoto Yatima katika kituo cha kulea watoto Yatima kilchopo kijiji cha Ibumila halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo wakiwa katika eneo La igima wakakutwa na ajali iliyohusisha roli ya mizigo aina HOWO lenye nambari za usajiri T108DYD na basi aina ya kosta lenye no 287.
Ni nyimbo za simanzi zinazoendelea katika misa ya kuaga miili ya wanauvikanjo 9 katika kanisa katoric la mtakatifu Yoseph Jimbo la Njombe ambavyo vimetokana na ajli iliyocha majeruhi wengine 18 wanaoendelea na matibabu katika hospitali za Kibena,Ikelu na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya .
Tukio hilo limeacha msiba mzito na simanzi kwa kanisa na wakazi wa mkoa wa Njombe kwa ujumla jambo ambalo linamuibua mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba kueleza jitihada zinazochukuliwa punde baada ya kupokea taarifa za ajali na kisha kutoa kauli ya matumaini kutoka kwa rais kwa wananchi mbele ya madhabahu .
Awali akieleza historia ya mkasa huo uliacha hisia kwa kanisa Padre Ausebius Kyando anasema tukio baya limewakuta wakifanya matendo ya kitume kwa wahitaji huku Askofu John Ndimbo ambaye ni msimamizi wa kitume kutoka jimbo katoriki Njombe akisema tunapaswa kujitathimini tunaicha dunia tukiwa katika mazingira gani.
Waumini na wananchi wa mkoa wa Njombe nao akiwemo Edson Mtokoma wametoa hisia zao kwa msiba huo ambapo wanasema wameondokewa na watu mahili na muhimu katika imani na kijamii.