NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi, Tawi la Benki Kuu ya Tanzania Dodoma, Bw. Abel Sahani,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango kutoka Zanzibar,Aboud Mwinyi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) Beng’i Issa,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Taifa ya Huduma Jumuishi za Fedha Betrida Wilfred,akielezea kitabu kilivyoandikwa na malengo ya Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande ,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande ,akionyesha kitabu baada ya kuzindua Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju na kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe. Hamad Hassan Chande ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) hafla iliyofanyika leo April 25,2022 jijini Dodoma yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.
………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande,ameiagiza Kamati ya Wanawake ya Huduma Jumuishi za Fedha (WACFI) kwenda kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi ili kuwasaidia wanawake katika huduma jumuishi za fedha.
Naibu Chande ametoa agizo hilo leo April 25,2022 jijini Dodoma wakati akiizidua Kamati hiyo yenye wajumbe 22 kutoka wizara mbalimbali za Serikali ,Taassi na Asasi za kiraia inayolenga kuongeza idadi ya wanawake katika sekta ya fedha.
Naibu Waziri Chande ameiagiza Kamati hiyo kuhakikisha inawafikia pia na kuwaelimisha wanawake hasa waishio vijijini ili nao wawe ni miongoni mwa watumiaji wa huduma rasmi za fedha.
Amesema kuwa wananchi waishio vijijini ni asilimia 8.6 tu ndio wanaopata huduma za benki ikilinganishwa na asilimia 32.1 ya wale wanaoishi mjini.
“Kuna umuhimu kwa wanawake kupewa elimu ya namna ya kuweka akiba, kufanya uwekezaji, kukata bima na kujiandaa na maisha ya uzeeni,ipo haja ya kuwahamasisha wadau wa sekta ya fedha kupendekeza mikakati itakayoongeza upatikanaji wa takwimu za kijinsia hasa kutoka kwa sekta binafsi ili zitusaidie kufanya maamuzi ya kisera kwa kuzingatia usawa wa kijinsia,”amesema.
Amesema kuwa kamati hiyo imelenga kuhakikisha wanawake nchini wanafikiwa na kutumia huduma rasmi za fedha na kuhakikisha usawa wa ufikiaji wa huduma hizo kati ya mwanamke na mwanaume.
“Wanakamati nimeambiwa mpo 22, mliochaguliwa lazima mhakikishe kuwa manakwenda kufanya kazi ili waliowachagua kuendelea kuwaamini mkasaidie wanawake kufikiwa na huduma jumuishi za fedha ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa waliopo vijijini”amesema Mhe.Chande
Chande amesema hatua hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa mikakati ya Mpango wa Pili wa huduma Jumuishi za Fedha unaolenga kujumuisha zaidi kundi la wanawake katika matumizi ya huduma rasmi za fedha nchini.
Amesema,suala la kuinua wanawake kiuchumi kwa kuongeza ushiriki wao katika sekta ya fedha ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapindunzi ya mwaka 2020, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 -2025/26) na Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa mwaka 2020/21-2029/30.
“Kamati hii ni muhimu na inajukumu kubwa katika kubuni, kuchochea na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mikakati inayolenga kuongeza idadi ya wanawake katika kuzifikia na kuzitumia huduma rasmi za fedha na hatimaye kunyanyua kipato cha mwanamke
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema kuwa huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM na kutekeleza dhamira thabiti ya Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mwanamke kinara katika masuala ya kiuchumi kwa wanawake .
Awali Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Florens Luoga, amesema pamoja na wanawake kuwa na uwezo mkubwa wa kujiweka akiba kuliko wanaume bado wanahifadhi sehemu zisizo rasmi zinazohatarisha usalama wa hakiba zao.
Prof.Luoga amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa wanawake ndiyo wamekuwa na uwezo wa kuweka akika zaidi ukilinganisha na wanaume lakini maeneo wanahifadhi siyo rasmi.
“Wanawake ndiyo wenye uwezo mkubwa wa kuweka akiba kuliko wanaume lakini sehemu wanazoweka akiba hizo mara nyingi ni majumbani eneo ambalo siyo rasmi lakini pia wakitaka kukopa wanatafuta rafiki ili amkopeshe na siyo katika taasisi rasmi za kifedha”amesema Prof.Luoga
Aidha, amesema vikundi vingi vya kuweka akiba na kukopa nchini ni vya akinamama lakini namna vinavyoendesha vinaweza visiwe na tija kwao.
“Ni vizuri kama vinaweza kuandaliwa vizuri tukatafuta namna ya kuviweka ili akinamama siyo tuu kupata huduma bali huduma za fedha jumuishi zikaimarishwa ili kuwafikia wananchi wote”ameeleza
Pia amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya kufikisha huduma jumuishi za fedha kila eneo na kuwafikia watu wote wakiwemo wanawake.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Beng’i Issa, amesema kuwa kamati hiyo ipo tayari kwenda kutekeleza majukumu yake ya kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa wanawake nchini.