Na Eleuteri Mangi, WUSM-Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu Aprili 25, 2022 amekagua ujenzi wa jengo la wizara hiyo linalojengwa katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, Bw. Yakubu amemsisitiza mkandarasi wa jengo hilo kwenda na kasi ya Serikali kukamilisha ujenzi huo kama ilivyopangwa ili jengo hilo likamilike kwa wakati mujibu wa ratiba ilivyopangwa ndani ya miaka miwili tangu kusainiwa mkataba wa makubaliano mwaka jana.
Mkataba wa ujenzi wa jengo hilo ulisainiwa Septemba 22, 2021 jijini Dodoma kati ya Kati Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi kwa niaba ya Wizara hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani kwa niaba ya shirika hilo.
Jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa sita litagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 22.843 hadi kukamilika kwake na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni watekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni wasanifu na wabunifu wa jengo halo.