Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara ,Abdulrahman Kinana amewapa onyo wagombea wa chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama ,wasitafute uongozi kwa Umaarufu wala fedha zao kwani kura hazinunuliwi.
Amezitaka kamati za siasa za mkoa,wilaya kutoona aibu wala Aya kuwakata majina wale watakaobainika kucheza rafu za rushwa.
Akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM Mkuranga,baada ya kutoka kuzindua ujenzi wa tawi la Mwanambaya Kinana ,aliwataka wanachama waamue wenyewe kuchagua viongozi bora na si Bora kiongozi.
Pia alikemea mchezo wa kuchafuana ili mwingine ashindwe kugombea,na kuongeza kamati za siasa zinataarifa za kina watu wasipotoshane na kuchafuana.
“Kuchafuana hapana, kubebana hapana,tafuteni uongozi kwa haki sio kutafuta viongozi wako wa matawi,mashina kwa Ajili ya uchaguzi wa baadae”
“Siku zote hawawatambui,huusalimii,huna habari nao, Uchaguzi ukifika ndio unapitapita kutumia umaarufu, Kila mwanachama ana haki ya kugombea na kuchagua na sio kununuliwa,”:Mnakubaliana na Mimi”;!
Kinana alieleza, kabla ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti,aliitwa na Rais,na baada ya kukubali,agizo la kwanza alilopewa ni kusimamia uchaguzi kikamilifu.
“Mwenyekiti aliniambia nihakikishe uchaguzi unafanyika kwa Uhuru na haki,Nitasimamia hilo”
Vilevile Kinana alibainisha kuwa, ukitaka uadilifu lazima CCM iwe mfano, Chama hicho kimepewa ridhaa moja kuwa na sikilo la kusikiliza changamoto na kero za wananchi ili zifikishwe sehemu husika.
“Wananchi wanadhulumiwa tunanyamaza,tusinyamaze tuwasemee na tuna kazi kubwa ya kusemea mazuri inayofanya Serikali ,nampongeza Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge,Kaeleza yote yanayotekelezwa na Serikali na fedha walizopokea kutoka Serikali na namna zilivyotumika:'”Naomba na Anachoomba Rais kuungwa mkono,kupewa moyo”aliongeza Kinana.
Hakusita kuwapongeza wakurugenzi wa Halmashauri, viongozi wa matawi ,kata na madiwani na mabalozi ambao wanajitolea licha ya kufanya kazi kubwa .
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Saidi Goha Alieleza Mkoa una mashina 7,205 kati ya hayo 3,239 yameshafanya uchaguzi na 1,056 michakato inaendelea ili kufanya uchaguzi.
Goha alielezea kwamba Hali ya kisiasa Ni shwari, Utekelezaji wa ilani unaendelea vizuri ikiwemo sekta ya elimu wanafunzi walikuwa wakisoma kwa shida kutokana na uchache wa madarasa ,wananchi walichangishwa lakini kufikia 2022 kadhia hii imeondoka .
Kwenye vitega uchumi alisema ,lengo kumalizia ujenzi wa ukumbi Kama kitega uchumi vya Chama na Sasa imefikia asilimia 75 ,mpango uliopo wamejipanga kukopa fedha katika mfuko wa Chama ili ukumbi uweze kukamilika .
Alimshukuru Kinana kwa kufika kufanya ziara Mkoani hapo ikiwa Ni mkoa wa kwanza tangu achaguliwe na Ni siku ya 24 tangu achaguliwe.
Akitoa salamu za Serikali,mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge alisema ,2020-2025 inaendelea kutekeleza ilani ya CCM.
Akizungumzia sekta ya elimu alisema, wanaendelea kuboresha miundombinu ya madarasa ambapo Bilioni 17.1 zimetumika kujenga madarasa 108 ,huku Bilioni 8.4 zimetumika katika ujenzi wa Madarasa 422 ya Sekondari.
“Pia matundu ya vyoo 540 ,shule mpya 12 kwa Bilioni 5.64 ambazo zimeshatolewa .
Katika afya , Kunenge alieleza Kuna vituo vya afya 434 kimkoa na Kuna fedha Jumla ya sh.bilioni 2.3 zilitolewa kupitia Tozo kwa Ajili ya ujenzi wa vituo vya afya Tisa.
Kuhusu Viwanda Kunenge, alinijinasibu mkoa huo ni ukanda wa viwanda na unaongoza katika ambapo una viwanda 1,453 kati ya hivyo 87 Ni vikubwa .
Aliishukuru kwa Serikali ya awamu ya sita kufungua miundombinu ya barabara ,ukiangalia bararaba ya Chalinze-Morogoro upembuzi yakinifu unaendelea kwa Ajili ya kuendeleza upanuzi wa ujenzi ,pia Mlandizi -Mzenga-selous ambapo jitihada zinaendelea na itakuwa barabara muhimu na ile ya Madafu-mksigusugu km.12.5.
“Barabara hizi zitasaidia kuleta Imani kwa wawekezaji kuona fursa ipo Mkoani Pwani kwa kupunguza changamoto za Kero ya miundombinu korofi.”Kunenge alifafanua.
Sekta ya maji , Kunenge alibainisha DAWASA imepokea Bilioni 228 kwa Ajili ya maji kati ya hizo zinatekeleza miradi mikubwa kumi ambapo ikikamilika itanufaisha Wakazi 834,000 na ile ya RUWASA ikikamilika itanufaisha wakazi 99,334.
“Nawapongeza Taasisi hizi kwani zimejipanga kufikia asilimia 95 kabla ya muda uliolengwa na kupangwa ili kupunguza kero ya Ukosefu wa maji “alisema Kunenge.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega alisema bado Kuna kazi kubwa ya kufungua miundombinu ya barabara Vijijini , ikiwemo Mjini Mkuranga-Kisiju katika bandari iliyojengwa toka enzi za ukoloni.
Alielezaa bandari ile haifi na wanaomba awe balozi wakati akitaja bandari zote asisite kuitaja ya Kisiju kwani inategemewa na wananchi Hadi wa Mafia.
Ulega aliomba barabara ya Mkuranga-Kongowe ipanuliwe ili kupunguza ajali na kusema , upo mradi mkubwa wa kimkakati Stendi ya mabus makubwa wanatarajia kuuita Samia Suluhu Hassan na habari za matumaini kwa wananchi ni kuwa mradi huo ukwenda kumalizika .
“Nakushukuru kwa ziara hii kufanyika Mkuranga ,umetufanyia kazi kubwa na kuacha Alama pale ulipofungua ujenzi wa tawi la Mwanambaya ambako Mimi naishi”alisisitiza Ulega .
Alimshukuru Rais kwa kazi aliyofanya mwaka mmoja kwa kutoa fedha nyingi za Uviko kujenga madarasa pamoja na miundombinu ya barabara .
Mwenyekiti wa CCM Pwani Ramadhani Maneno, Anaeleza juu ya Chalinze kuwa wilaya , amemuomba Kinana kuchukua nafasi kukaa na Mwenyekiti CCM Taifa kurejea kauli ya Rais wa awamu ya tano marehemu John Magufuli aliyowaambia wana Chalinze .
Maneno alisema Chalinze ni kubwa, vigezo vinazingatiwa japo igawanywe iwe ya kichama kama si Serikali.
Alimtoa hofu mkuu wa mkoa wa Pwani,kumsaidia anapochukua Maamuzi mazito kwani wapo baadhi wanachafua Serikali kwa mwamvuli na kisingizio cha