Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wana CCM wa mkoa wa Tanga akiwa katika ziara ya kujitambulisha mara baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Chama hicho.
…………………………………
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka madiwani na wabunge kukataa kupitisha miswada ya Sheria yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.
Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.
Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.
“Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.
“Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano…sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na wananchi,” alisema.
#CCMImara
#KaziIendelee
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akiangalia Ngoma wakati alipowasili kwenye mkutano wa Wana CCM mkoani Tanga Leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akizungumza na mmoja wa wazee wa CCM waliofiks kumlaki alipwasili mjini Tanga.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wana CCM mkoani Tanga Leo.
Wabunge wa mkoa wa Tanga wakiwa katika mkutano huo kulia ni Khamis Mwijuma mbunge wa Muheza na kati ni Mbunge wa Jimbo la Bumbili Januari Makamba