Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa (CCM)
Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa (CCM)
Mohamed Hassan Moyo aliwataka vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea
mafanikio ya muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote
ilivyofanya kazi kuleta maendeleo.
Akizungumza kwenye kongamano maalumu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
mkoa wa iringa (UVCCM),Moyo alisema kuwa kumeibuka wimbi la watu ambao wanataka
kuuvunja muungano kwa maslai yao.
Alisema wapo watu hawataki kuona muungano huo ukiendelea kuimarika hivyo
jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wanapaswa kuendelea kuulinda
muungano ili usivunjike.
Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa
kuuvunja muungano kwa nia ovu zao hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda
muungano.
Aidha Moyo aliwataka vijana wa chama hicho wanaoenda kugombea nafasi mbalimbali
za uongozi kwenda kushiriki uchaguzi kwa uadilifu ili kupata viongozi walio
imara na bora kukiongoza chama hicho.
Alisema kuwa vijana wanaoenda kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio
mamluki wanaopandikizwa kwa lengo la kuja kukivuruga chama hicho hivyo
wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za chama.
Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona
wagombea wanashinda kwa kutoa rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.
Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama
hicho kwa mafanikio ya kukivusha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo
chama hicho kitashiriki kutafuta mamlaka ya kuunda serikali.
kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa Vijana
(UVCCM) taifa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Kenani Kihongosi
alisema kuwa katiba ya chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki
ya kugombea nafasi yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.
Kihongosi aliwata vijana wa UVCCM kuacha tabia ya kulalamika kuwa wananyimwa
nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao hawajitokezi kugombea.
Kihongosi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan anawaamini vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za
serikali,ameteua Zaidi ya asilimia 75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza
serikali ya awamu ya sita.
Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM Tanzania kuacha mara moja kuwabeba
wagombea,waache wanachama waamue nani anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho
ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.
Kihongosi alisema kuwa hataki kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali
fomu zote zinatakiwa kufika sehemu husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi
kwa mjibu wa katiba ya chama.
Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama
hicho ili kupata viongozi bora ambao wataweza kukiongoza chama hicho na
wanachama chake kwa kuwa rushwa haina nafasi mwaka huu.
Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu
vijana wenzao ili kila mmoja apate nafasi anayostahili kulingana na nafasi
anayoishika naanayoigombea.
“Ni marufuku kwa viongozi kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa
kufanya hivyo kutapekea chama kupata viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa
viongozi” alisema Kihongosi
Kihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea nafasi mbalimbali
kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.