Mgeni wa Heshima mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wajumbe wa chanjo ya polio Manispaa ya Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa kupitia
idara ya afya Inatarajia kutoa chanjo ya Ugonjwa wa polio kwa watoto 25 elfu
walio chini ya umri wa miaka mitano (5) ili kuwakinga na hatari ya kuambukizwa
virusi vya maradhi hayo
Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr. Baraka alisema
kuwa Halmashauri hiyo tayari imepokea dozi 27 elfu za kinga ya Polio na kwamba
zoezi la chanjo litaanza kutekelezwa kuanzia April 28 hadi mei mosi mwaka huu.
Wakati wa mafunzo kwa kamati ya msingi ya
huduma za afya kwa jamii Mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo amehimiza viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa
chanjo hiyo kwa watoto.
Dr. Chaula alisema kuwa lengo la kutoa mafunzo
hayo ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya umuhimu wa wazazi na jamii kwa
ujumla juu ya kuwapatia chanjo ya polio watoto wao.
Alisema kuwa ugonjwa wa polio unataja kuathiri
watoto wenye umri wa miaka chini ya kumi na nne lakini kwa mujibu wa wataalam
wa afya ugonjwa huo uathiri zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka mitano
Dr. Chaula alisema kuwa tayari chanjo
zimekuwishapokelewa katika manispaa ya Iringa kilichosalioa ni utekelezwaji wa
zoezi lakutoa chanjo kwa wahusika
Mganga mkuu wa Manispaaya Iringa ameyasema
haya wakatiwa akimkaribisha mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo katika uzinduzi wa kampeni hiyo yaChanjo.
Kwa upande wake mgeni wa Heshima mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ni lazima kuwashilikisha viongozi
wa mitaa ili waone umuhimu wa jambo hilo.
Alisema kuwa kuwashirikisha viongozi wa ngazi
ya mtaa hadi kata kutasaidia kufanikisha zoezi hilo la chanjo ya polio kwa
watoto wadogo na jamii kulijua swala hilo la polio.
Moyo aliwaomba viongozi wa dini wilaya ya
Iringa kulichukua swala la polio kama la kwao kwa kuwaelimisha jamii juu ya
chanjo ya polio kuwa ni chanjo salama ambayo inawakinga woto wao.
Aliwaomba wananchi kushiriki katika kampeni ya
chanjo ya polio kwa watoto wadogo ambao ndio waathirika wakubwa na chanjo hizo
zipo kwa ajili ya kuwakinga watoto wao.
Mkuu huyo wa wilaya alimazia kwa kumuagiza
mganga mkuu wa manispaa ya Iringa kuhakikisha anaishirikisha jamii na viongozi
wa dini na viongozi wa kimila ili waweze kusaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi
husika.