Katibu mkuu wa umoja wa Vijana
(UVCCM) taifa Kenani Kihongosi akiongea na vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi
Baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa wakimsikiliza katibu mkuu wa UVCCM taifa Kenani Kihongosi
Na Fredy Mgunda,Iringa.
KATIBU mkuu wa umoja wa Vijana
(UVCCM) taifa Kenani Kihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea
nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.
Kihongosi alisema kuwa katiba ya
chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki ya kugombea nafasi
yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.
Akizungumza wakati wa kongamano
maalum la umoja wa vijana mkoa wa Iringa(UVCCM) kuacha tabia ya kulalamika kuwa
wananyimwa nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao
hawajitokezi kugombea.
Kihongosi alisema kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawaamini
vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za serikali,ameteua Zaidi ya asilimia
75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza serikali ya awamu ya sita.
Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM
Tanzania kuacha mara moja kuwabeba wagombea,waache wanachama waamue nani
anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya
hiyo na chama kwa ujumla.
Kihongosi alisema kuwa hataki
kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali fomu zote zinatakiwa kufika sehemu
husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi kwa mjibu wa katiba ya chama.
Alisema kuwa katika uchaguzi wa
mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama hicho ili kupata viongozi bora
ambao wataweza kukiongoza chama hicho na wanachama chake kwa kuwa rushwa haina
nafasi mwaka huu.
Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa
umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu vijana wenzao ili kila mmoja apate
nafasi anayostahili kulingana na nafasi anayoishika naanayoigombea.
“Ni marufuku kwa viongozi kupanga
safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo kutapekea chama kupata
viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa viongozi” alisema Kihongosi
Alisema kuwa mwaka huu ni mwaka wa
zoezi la SENSA hivyo wananchi wote wanatakiwa kujitokeza,kuhimizana na
kujitokeza kuhesabiwa wakati ukifika ili serikali iweze kujua namna ya kupanga
bajeti na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.
Kihongosi alisema kuwa vijana
wanawajibu wa kujitokeza kuhesabiwa na kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza
kuhesabiwa wakati wa zoezi la SENSA.
Kwa upande wake Katibu wa ccm mkoa
wa Iringa Rukia Mkindu amewataka vijana wa umoja wa chama cha mapinduzi mkoa wa
Iringa (UVCCM) kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kuanzia
ngazi ya shina hadi taifa kwa lengo la kuongeza chama hicho.
Mkindu aliwaomba vijana hao kuwa
wanapoenda kugombea kuacha tabia ya kupokea na kutoa rushwa kwa kufanya hivyo
kutatoa viongozi ambao sio bora kukiongoza chama hicho hapo baadae.
Aidha katibu wa Iringa Mkindu
alitumia muda huo kumpongeza katibu mkuu wa umoja wa vijana taifa Kenani
Kihongosi kwa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu na kufanya kazi kubwa katika umoja
huo kwa muda mfupi alipochaguliwa kuwa kiongozi.
Mkindu alimazia kwa kupongeza kazi
kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa
mkoa wa Iringa.
Naye Mkuu wa wilaya ambaye ni
kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliwataka
vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea mafanikio ya muungano wa
Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote ilivyofanya kazi kuleta
maendeleo.
Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu
wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa kuuvunja muungano kwa nia ovu zao
hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda muungano.
Alisema kuwa vijana wanaoenda
kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio mamluki wanaopandikizwa kwa lengo
la kuja kukivuruga chama hicho hivyo wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za
chama.
Moyo alisema kuwa uongozi wa
serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona wagombea wanashinda kwa kutoa
rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.
Alisema lengo la uchaguzi huo ni
kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama hicho kwa mafanikio ya kukivusha
chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo chama hicho kitashiriki kutafuta
mamlaka ya kuunda serikali.