***********
TAASISI inayojishughulisha na Uwekezaji katika Kilimo nchini (JATU PLC) imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha uzinduzi wa filamu ya ‘Royal Tour’ na kusisitiza kuwa itazidi kulitangaza Taifa la Tanzania Duniani.
Akizungumza Dar es Salaam siku chache baada tangu kuzinduliwa rasmi kwa filamu hiyo katika Jiji la New York nchini Marekani, Meneja wa Jatu Mohamed Simbano amesema kwa kufanikisha hatua hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan anazidi kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kuiletea maendeleo Tanzania.
“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ukweli anazidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa hili kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani, Mungu aendelee kumlinda na kumsimamia”, amesema Simbano.
Amesema kuzinduliwa kwa filamu hiyo inayoonyesha vivutio mbalimbali vya utalii na kitamaduni, kutazidi kuongeza idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini kwa lengo la kuja kuvitazama hatua ambayo itasaidia kukuza pato la Taifa kutokana na fedha za kigeni