Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara yake, katika Kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Naibu Waziri, Jumanne Sagini, Wapili kulia ni Katibu Mkuu, Christopher Kadio, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokua akizungumza katika kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Naibu Waziri, Jumanne Sagini, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kulia), na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kushoto), kabla ya kuanza kwa kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akisalimiana na Katibu Mkuu, Christopher Kadio, na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), wakati alipokua anawasili katika kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara yake (hawapo pichani), katika Kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika Kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika Kikao cha kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Randama ya Bajeti ya Wizara yake, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.