Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka, akisalimiana na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose. baada ya kufika ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya mazungumzo, Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia, mara baada ya kuwasili ofisini kwake akiambatana maofisa waandamizi wa Kampuni hiyo ili kufanya mazungumzo nae.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose, akizungumza na mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka akizungumza na ugeni wake ofisini kwake
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose(kulia) akizungumza na watendaji wakuu wa Vodacom alioongozana nao mara baada ya kutoka ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose, akizungumza na wafanyakazi wa Vodacom kanda ya Kati jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose, akisalimiana na wanafunzi wa kidato cha tatu na tano wa shule ya sekondari Dodoma mara baada ya kuwasili shuleni hapo na ujumbe wake.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose, akiwaelezea wanafunzi wa shule ya sekondari Dodoma kuhusu namna tovuti ya e-fahamu inavyofanya kazi baada ya kuitembelea shule hiyo akiwa na ujumbe wake, ikiwa sehemu ya ziara ya kutembelea na kujua maendeleo ya huduma za kidijitali mashuleni kupitia vifaa vilivyotolewa na kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na uongozi wa shule ya Sekondari Dodoma mara baada ya kuwasili shuleni hapo.