Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi pamoja na watendaji wa mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya Mawaziri wa Kisekta kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 20 April 2022.
Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha kilichofanyika mkoani Arusha tarehe 20 April 2022.
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akuzungumza katika kikao kati ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akuzungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Meryprisca Mahundi akuzungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022Niabu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza Chillo akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022.Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande akuzungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akuzungumza katika kikao kati ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akuzungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022.
******************
Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA
jumla ya vijiji 75 vilivyokuwa na migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa wa Arusha vimenufaika na hisani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kwake kubaki maeneo yake kufuatia vijiji hivyo kuingia kwenye migogoro ya matumizi ya ardhi na maeneo ya hifadhi.
Mkoa wa Arusha unahusisha vijiji na mitaa 116 kati ya 975 vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi na hifadhi, mashamba, ranchi, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambapo taarifa yenye mapendekezo ya utatuzi wake iliwasilishwa serikalini tarehe 23 Septemba 2019 na kutolewa uamuzi na Baraza la Mawaziri.
Katika taarifa hiyo ilipendekezwa vijiji 920 kati ya 975 vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi nchini kubaki ingawa baadhi yake vitahusisha marekebisho ya mipaka kwa njia shirikishi na baadhi yake migogoro yake ilishatatuliwa.
“vijiji na mitaa 116 Arusha kuachiwa vijiji 75 kubaki kwenye maeneo yake ni hisani ya kipekee na tunatakiwa tuiheshimu na tusiitumie vinginevyo kwa sanababu Mhe. Rais Samia alikuwa na uwezo wa kutaka kuviondoa lakini ameridhia maeneo 75 kubaki” alisema Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.
Akizungumza na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 April 2022 wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta mkoani humo, Dkt Mabula alisema, sambamba na uamuzi wa serikali, uongozi wa mkoa utakuwa na jukumu la kusimamia mpango wa matumizi ya ardhi sambamba kudhibiti vyanzo na vichocheo vyote vya kuzalisha migogoro.
“Natambua mkoa wa Arusha unazo changamoto nyingi zinazosababishwa na muingiliano wa matumizi ya ardhi lakini niwakumbushe kuweka utaratibu mzuri wa utekelezaji uamuzi wa serikali unaohusu migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini” alisema Dkt Mabula.
Kwa upande wao, Mawaziri wa Wizara za Kisekta walihimiza umuhimu wa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi chini kusimamia vyema utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila kuleta taharuki kwa wananchi sambamba na kuhakikisha maeneo ya hifadhi yanatunzwa.
‘’Kama Wizara ya Kilimo tupo katika mchakato wa kutunga sheria ya kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi kutenga na kubaini maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kilimo ili kuondoa migogoro ya ardhi’’ alisema Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega alisema, uzoefu unaonesha kuwa maeneo mengi yaliyoathirika na uvamizi ni ya mifugo na kusisitiza kuwa maeneo hayo ni ranchi zinazotumika pia kama ardhi ya akiba na kuweka wazi kuwa, hakuna namna yoyote maeneo hayo kutoonekana vichaka.
Tayari Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta katika awamu ya pili ya kupeleka mrejesho wa maamuzi ya baraza la Mawaziri kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 imeshatembelea mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mara na Arusha.