Msanii maarufu wa nyimbo za asili kabila la wasukuma Edward Ntemi aliefariki Dunia Aprili 18,2022 atazikwa Aprili 26 mwaka huu.
Alie kuwa msanii maarufu wa nyimbo za asili kabila la wasukuma Edward Ntemi afariki Dunia Aprili 18,2022 .
***************************
Na Hellen Mtereko MWANZA.
MSANII wa ngoma za kabila la Wasukuma Edward Mashiku Ntemi ambaye ndiye mwalimu wa kwanza kuwafundisha Wanzungu kucheza ngoma,kuimba na kuongea Lugha ya asili ya Kisukuma nchini Denmark,amefarki dunia.
Akizungumza kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu Paulo Lusana alisema baba yake mzee Mashiku alifariki Dunia April 18 mwaka huu majira ya saa 10:47 asubuhi nyumbani kwake Kisesa Bujora wilayni Magu mkoani Mwanza kutoka na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya Ini.
“Marehemu Edward Ntemi alianza kuugua mwaka 2021 akiwa nchini Denmark, tulimpeleka kupata matibabu na majibu yalionyesha anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya Ini ndipo tulipoamua kumrudisha nyumbani nchini Tanzania Novemba mwaka jana na kuendelea na tiba mubadala za miti shamba baada ya yeye kuhitaji a”alisema Paulo.
Alisema,kati ya mwaka 1979/ 19780 Msanii Mashiku alialikwa kwenda Denmark Copenhagen kwenye kongamano la muziki na alifanya vizuri hadi kuwavutia Wazungu ,kuifanya jamii hiyo kupenda ngoma za asili ya Kisukuma, Lugha yake kwa ujumla na ikapata heshima ulimwenguni.
“Mashiku ndiye aliyefanya Wazungu kuja Tanzania hususani Makumbusho ya Bujora ili wajifunze mambo mengi ya kabila,mila na desturi za Wasukuma,kufuatia yeye kufanya maonyesho ya tamaduni, maisha na majina ya Kisukuma walipewa Wazungu katika miji mbali,”alisema Paulo.
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mtakatifu Sesilia Bujora Lucy Sospeter alisema,kifo cha Edward Mashiku ambaye ni mwalimu wao wa kwanza na nimwanzilishi wa kuitangaza Tanzania kupitia ngoma za Bugobhogobho ambayo ni asili ya mila na desturi za Wasukuma,nipengo kubwa kwao.
“Tutamkumbuka sana mwalimu wetu wakwanza katika kutufunfisha ngoma za kitamaduni ya Kisukuma,ingawa alikuwa anaishi Denmark ambako alitumwa na mlezi wetu marehemu Padri Celement kwenda kufundisha tamaduni za Kisukuma kupitia ngoma mbalimbali za kabila hilo,alikuwa akirudi Tanzania na kujumuika nasi,”alisema Lucy.