***************************
Pata amani ya moyo ukiwa umebima gari lako kupitia Benki ya NMB.
- Unaweza kupata mkopo wa bima na kuulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi 10
- Janga litakapotokea, watasimamia na kuhakikisha madai yako yanalipwa ndani ya muda mfupi.
- Utapata huduma kwenye matawi yote ya NMB yaliyotapakaa nchi nzima
Kwa kuendelea kuwajali na kuwathamini Watanzania, Benki ya NMB ikishirikiana na makampuni ya Bima, inatoa huduma ya bima ya gari au chombo cha moto (gari, pikipiki n.k) kwa lengo la kutoa kinga dhidi ya hasara itokanayo na ajali, wizi, uharibifu na majeraha ya mwili/ kifo kwa mtu mwingine.
Kuna aina mbili za bima hii, ndogo na kubwa. Bima ndogo (third party only) ina mkinga mwenye chombo dhidi ya majanga yaliyosababishwa kwa watumiaji wengine wa barabara ambayo ni kifo/majeruhi na uharibifu wa mali zao.
Wakati, Bima kubwa (comprehensive) inakinga uharibifu wa gari ya mteja kutokana na majanga ya barabarani, moto, wizi wa gari, mafuriko,kimbunga na majanga yote yanayofidiwa na Bima ndogo.
Unachohitaji ni;
- Nakala ya kadi ya chombo na kitambulisho halali
- Picha za chombo kwa wakati huo
- Thamani ya chombo
Kata Bima hii kupitia *150*68# na endapo utahitaji kutoa taarifa za madai, basi fika tawi la NMB karibu yako au piga simu nambari 0800 002 002 bure kabisa!
Kwa barua pepe, tuma kwenda [email protected]
Umebima- SiNgumuKihivyo!