**********
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameshiriki mazishi ya Msanii Maunda Zoro, yaliyofanyika Toangoma, Kigamboni Dar es Salaam, (leo) Jumamosi 16 April 2022.
Katika mazishi hayo, Shaka alijumuika na wanafamilia na waombolezaji, ndugu jamaa na marafiki ambapo alipata nafasi ya kuwasilisha salamu za pole na mkono wa rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
*”Mhe Rais Samia yuko safari (ziara) amenituma nifikishe salamu zake za pole kwenu ndugu, familia, jamaa na marafiki sambamba na kuwasilisha mkono wa rambi rambi toka kwake, anatambua kuwa tasnia hii imepoteza msanii mahiri ambaye wakati wote wa uhai wake aliitumia Sanaa kufikisha ujumbe , kuburudisha, kuhamasisha na wakati mwingine kuiunganisha jamii kwa ujumbe, sambamba na kuenzi kipaji cha (babake) Mzee Zahiri Zoro lakini Maunda akiwa msanii anaechipukia alifanya vizuri sana”* alisema Shaka katika sehemu ya maelezo yake.
Bwana Ametoa , Bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe
Apumzike kwa Amani Maunda Zoro.
Ameen.