************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema zao la kibiashara la korosho linaendana na mnyororo wa thamani,hivyo wale viongozi watakaoshindwa kupata tija na matokeo kwenye zao Hilo watakuwa wanahujumu na hawatoshi.
Ameeleza iwe viongozi wa Serikali ama chama wajibu mkubwa ni kusimamia kero ya wananchi wakiwemo wakulima .
Akizindua kampeni ya kupalilia mashamba ya korosho Mkoani Pwani, Kunenge ameeleza haiwezekani mkuu wa mkoa ama mkuu wa wilaya anatoka ofisini kwenda kusimamia usafi wa mashamba kwenye maeneo ya viongozi ambao wapo lakini hawatimizi wajibu wao.
“Tukiona eneo kilimo cha zao lolote ama korosho mambo hayaendi Lazima tuulizane vizuri, upande wa Chama tuulizane unafanya nini, kwasababu kiongozi wa chama uhalali wake ni Wananchi”
“Cheo chako kinatokana na watu,kama huwezi kuwasimamia hufai na hutoshi,;!”Kama ni kiongozi wa Serikali huko sehemu ukashindwa kusimamia utekelezaji wa ilani na majukumu yako hutoshi”
Kunenge alieleza, Vilevile mashamba yanatelekezwa ,tukipime na wahikikishe viuatilifu vinavyostahili vilivyo bora vinakuwepo kwa wakati na maofisa ugani watimize wajibu wao.
Alisema kuna sheria ndogondogo zilizo kwenye Maeneo mbalimbali zisimamiwe lengo zaidi kupunguza kero za wananchi.
Kwa upande wake, katibu Tawala msaidizi mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala alisema wameazimia kufanya kampeni hii kutokana na mashamba ya korosho kutelekezwa.
Alielekeza ni lazima yaandaliwe,yafufuliwe kwa maslahi ya wakulima wa zao Hilo, wilaya na mkoa na Taifa kijumla.
Twamala alibainisha,bodi ya korosho Tanzania kwa kumuunga mkono mkuu wa mkoa wa Pwani wamegawa maturubai ikiwa ni sehemu ya kuboresha kilimo hicho kwa tija.
Nae Fransis Alfred kutoka bodi ya korosho Tanzania,alisema Lengo la kampeni hiyo Ni kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 300,000 – 700,000 kufikia mwaka 2025-2026.
Pia kuongeza kiasi cha korosho ya kubanguliwa nchini kutoka wastani wa asilimia 10 ya uzalishaji hadi kufikia asilimia 60.
“Sambamba na hayo , kuhakikisha kunakuwa na soko endelevu na la uhakika kwa zao hilo la kibiashara.
Fransis aliipongeza mkoa wa Pwani,kwa ubora wa korosho kwa msimu huu ambapo Daraja la kwanza imefikia asilimia 72 kutokana na Hilo,bodi hiyo imetoa maturubai 102 kwa vyama vya msingi Mkoani hapo kwa ajili ya uangalizi mzuri wa korosho.
Baadhi ya wakulima akiwemo Otomaki Mosha, ameomba kuharakishwa kwa pembejeo ,viuatilifu wapate kwa wakati na kuomba wataalamu Kuwa karibu nao ili kuleta tija kwenye zao Hilo na wakulima kunufaika .