******************
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Chakula Duniani(*CFS*) *Ndg. Gabriel Ferrero de Loma-Osorio* na kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Kilimo nchini katika kufikia lengo la Ajenda 10/30.
Maeneo tuliyoyagusia;
Ujenzi wa maghala ya hifadhi ya mazao ya kilimo kuanzia ngazi ya Kijiji ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno.
2.Uboreshaji wa Maabara ya Afya ya Mimea na Viuatilifu iliyopo Arusha chini ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu(*TPHPA*) pamoja na kuwajengea uwezo zaidi wataalamu wa Mamlaka.
3.Program ya ushiriki wa Vijana katika Kilimo “_Building a Better Tomorrow”_ kwa lengo la kuwavutia vijana kushiriki katika sekta ya kilimo sambamba na utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa Ajira nchini.
4.Uwezekano wa Tanzania kuingia kama mwanachama katika Kamati ya Usalama wa Chakula Duniani(*CFS*)