Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0cm 5.4pt 0cm 5.4pt;
mso-para-margin-top:0cm;
mso-para-margin-right:0cm;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0cm;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Mwenyekiti
wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa makini kuisoma taarifa wakati wa ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Mwenyekiti
wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa makini kukagua miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Moja ya miradi ya kitua cha afya ambayo inaendelea kujengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Mwenyekiti
wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa
ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mwenyekiti
wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa akifanya kazi kwa mfano wakati wa
ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
KAMATI ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imesema haitaki kusikia maelezo ya
mchakato kwenye fedha za miradi ambazo zimetoka serikalini kwa wakati ili
kuharakisha kukamilisha miradi kwa haraka na kuanza kutumika kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua miradi ya halmashauri ya wilaya ya Iringa,mwenyekiti
wa kamati hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema
kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa ujenzi wa miradi kutokana na uzembe wa
wataalam.
Moyo
alisema kuwa fedha ambazo zimeletwa na serikali zinatakiwa zitumike kwa wakati
kulinga na majukumu ambayo yanatakiwa kutekelezwa kulingana na thamani ya fedha
ambazo zimeletwa kwenye miradi husika.
Alisema
kuwa fedha zikiwa zinaletwa kwenye miradi halafu hazitumiki kwenye miradi kwa
wakati zitaleta doa kwa halmashauri husika na kushindwa kupewa fedha nyingine
kwa ajili ya kutekeleza miradi mingine.
Moyo
aliwataka wataalam na wakandarasi kubadilika katika utendaji wao wa kazi ili
kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jitihada za
kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha
mkuu wa wilaya Mohamed Moyo alikemea vitendo vya baadhi ya wananchi kuiba vifaa
vya ujenzi jambo ambalo linakuwa linarudisha nyuma maendeleo ya ujenzi huo
hivyo serikali ya wilaya ya Iringa haitamvumia mtu yeyote atakaye hujumu miradi
ya maendeleo.
Moyo
alisema kuwa miradi yote inatekelezwa kwa ajili ya kusaidia juu za wananchi
katika kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika maeneo husika ambako
miradi inatekelezwa.
Alisema
kuwa miradi yote inatakiwa kutekelezwa usiku na mchana kwa kuwa fedha zipo na
zimetolewa kwa wakati kwenye miradi husika na kutekeleza miradi hiyo kwa
wakati.
Moyo
aliwataka wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuendelea kubuni vyanzo v
ipya vya mapato ya ndani ambavyo vitasaidia kuchochea maendeleo ya wananchi
katika halmashauri husika.
Kwa
upande wake kaimu Mhandisi ujenzi halmashauri ya wilaya ya Iringa Eng Nicos
Kasililika alisema kuwa wameyapokea maagizo yote ya kamati ya ulinzi na usalama
ya wilaya ya Iringa na kuahidi kuyafanyia kazi kwenye miradi yote
inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Eng
Kasililika alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imefanikiwa kutembelea
jumla ya miradi mitano inayotekelezwa kwa kutumia fedha kutoka serikali kuu
yenye lengo la kuchochea maendeleo kwa wananchi.