Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,Abubakari Kunenge ameagiza mabaraza ya ardhi kutimiza wajibu wao bila kuogopa mtu, Wala kundi kwani hakuna aliye juu ya sheria.
Aidha ameyataka kuacha kuruhusu mrundikano wa mashauri ,badala yake wajumbe wa mabaraza hayo wafanye Maamuzi kwa wakati bila kusuasua na watende haki kwa wananchi.
Kunenge alitoa maagizo hayo ,mjini Bagamoyo alipokuwa akiwaapisha wajumbe wa baraza la ardhi la Wilaya hiyo, ambapo aliwaasa wasitishwe ,wafanyekazi na Serikali ipo nyuma yao.
Aliwataka kujipima ili kuleta tija , watende haki , Vilevile wasionee mtu .
Alisema katika utawala wa sheria hakuna aliye juu ya sheria hivyo wajumbe walioapishwa wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ufahamu,ujuzi na utaalamu na kuishi kulingana na majukumu yao.
Pamoja na hayo,Alikemea baadhi ya viongozi wa Chama kuacha kushiriki kukumbatia wabadhilifu ,na kukemea wale wanaofanya dhuluma ,matapeli,kunyang’anya maeneo,kuvamia maeneo kuacha Mara moja na atakaebainika atashughulikiwa na avuliwe madaraka yake ikibidi aondolewe kwenye Chama.
“Mkoa umejipanga kuondoa migogoro ya ardhi ,sitopendelea ,mtu,sitoruhusu vimeseji ,Mimi sio wa hivyoo”: ,ukiwa katika Chama ,Serikali una chombo una mbadhilifu tutamshughulikia ,hatampendelea mtu ,tutatenda haki ,Tumechoka na migogoro ya ardhi “
” Nyinyi wajumbe wa mabaraza ya ardhi, Sitawauliza juu ya utendaji wenu ,nitajua ufanisi wenu kwa kuangalia kiwango gani mtatatua changamoto kwa jamii inayowazunguka na niwaambie hatutarajii tuwe na watu ambao hawatakuwa msaada. Tukiona hamna msaada tutawabadilisha” alifafanua Kunenge.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ,Zainabu Abdallah alibainisha kukosekana kwa baraza la ardhi ilikuwa kero kwa wananchi ambao walikuwa wanalazimika kwenda kibaha kufuatilia mashauri yao.
Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na nyumba wilaya ya Kibaha, Sara Mbuga ambaye alimwakilisha Msajili wa Mabaraza ya ardhi mikoa ya Pwani na Dar es salam aliwasihi wajumbe walioapishwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.
Kati ya Wilaya saba za Mkoa wa Pwani, wilaya tano zina Mabaraza ya Ardhi na Nyumba.