WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza leo April 11,2022 wakati akifungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani) leo April 11,2022 wakati akifungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) leo April 11,2022 wakati akifungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Ambaye pia ni katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka,akielezea lengo la Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza hilo Bw.Huruma Mageni,akizungumza wakati wa Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani)wakati akifungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Deus Seif,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) mara baada ya kufungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa Siku mbili jijini Dodoma.
……………………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ameagiza Mabaraza ya Vyuo Vikuu nchini kuhakikisha kunakuwepo na ubora kwenye elimu ya juu na yasishushe vigezo ili kupata watu wengi.
Prof.Mkenda ametoa kauli hiyo leo April 11,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo ambapo amewataka kuhakikisha wanapitia Mfumo mzima wa Elimu pamoja na Sera zake.
Amesema kuna baadhi ya vyuo shahada za walimu wake zinatia shaka na kusisitiza kuwa lazima elimu ya vyuo vikuu iangaliwe.
“Elimu ya juu iwe na viwango hata kama tunahitaji vyuo vingi zaidi lakini msukumo huu usitufanye tushushe viwango,”amesema.
Ameongeza “Sokoine iliangaliwa na Chuo Kikuu Dar es salaam sasa hivi mtu anataka atoboe hapo hapo aende, mtu hataki kuatamiwa kwasababu kuna baadhi ya vyuo hata degree za walimu zina mashaka, kuna chuo kilikuwa kinaongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo ambapo shahada yake inatokana na NGOs yaani zile degree ambazo zile unalipa kiasi fulani unapata degree, lakini ukiajiriwa tutakuuliza degree yako ni ipi? Ukiajiriwa na serikali tunataka kujua PhD yako ulipata wapi,”amesema.
Amehimiza kuongeza ubora wa elimu ili vijana wanaohitimu waajirike na kuajiri kwa kuwa na ujuzi wa kile walichosomea.
“Elimu ni uwekezaji wa vizazi na vizazi na uwekezaji huu ukifanywa vizuri tutakuwa tumewekeza katika maendeleo ya nchi,”amesema.
Aidha Prof.Mkenda amesema kuwa sera ya elimu ya mwaka 2014 inataka mtoto asome kwa miaka 10 elimu ya lazima suala hilo halijafutwa na kwamba sera hiyo ipitiwe na wakubaliane au wabadilishe sera.
“Sera ipo lazima tufanye maamuzi tunaitekeleza au hatutekelezi, kazi ya mitaala inafanyika vizuri, kwenye sera bado lazima tufikirie mtu akisoma kwa miaka saba akimaliza shule anaajirika au kujiajiri na ILO inasema anaajirika akiwa na miaka mingapi?…Tukipitia sera tutaangalia na sheria,”amesema Prof.Mkenda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Ambaye pia ni katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka amesema baraza hilo linajukumu la kuishauri Wizara na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yanafanyika kwa weledi huku akisisitiza kuwa Wizara imedhamiria kuinua ubora wa elimu.
”Baraza hilo lipo tayari katika kuhakikisha taratibu za Wafanyakazi na taratibu za uandaaji wa rasimu ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ya wizara hiyo unaendelea kujikita katika kuwekeza kwenye maboresho ya elimu lengo likiwa ni kuwatengeneza wataalamu wenye ubora kwa ajili ya kuwasaidia watanzaina.”amesema Prof.Sedoyeka
Naye Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Deus Seif,amesema kuwa bila kuwa na walimu wenye ubora katika Shule zetu tutaendelea kuzalisha watalaamu wasio na vigezo hivyo ni vyema kuhakikisha wanaotoa elimu kuwa na vigezo vya kutosha ili kusaidia hii taaluma inayotegemewa na taifa.
“Nataka niwahakikishie mwalimu akikosea gharama yake ni kubwa sana kuliko kosa kufanywa na daktari au Mhandisi kwa sababu unaweza kulirekebisha lakini kosa la mwalimu ni hatari sana,”Amesema Seif