Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma Manispaa ya Songea Kata ya Lilambo wameamua kujiunga na kazi ya ujenzi wa miradi mbalimbali kazi ambayo hufanywa mara nyingi na wanaume lakini wao wameamua kuvunja dhana hiyo kwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu la kazi ifanywe kwa bidii na waza.
Mmoja wa wanawake hao ni Tatu Mwamizi ambaye kazi yake kubwa ni kuchanga mchanga na kubeba kokoto anaeleza kwamba ujenzi wa miradi hiyo ya Rais Samia imewawezesha wanawake hao kusomesha watoto wao na pia kujikimu na hali ya maisha.
“Nikipata hela naweza kumnunulia mwanangu daftari, chakula ile akiba inayobakia namununulia sare za shule na kama kuna kifaa kimeisha,”
Naye Halima Mohamed anaeleza kwamba hapo awali hali yake ya maisha ilikua ngumu sana tifauti na sasa alipoanzamkufanya kazi ya ujenzi katika miradi hiyo iliyoanza hivi karibuni.
“Hali yangu kidogo kiugumu wa maisha nilikua nayumbayumba jinsi ya kumsomesha mwanangu lakini sasa hivi namshukuru Mungu hapa ninavyofanya kazi inanisaidia mwanangu anaendelea vizuri na mimi mwenyewe naendelea vizuri napambana na kazi,”
“Najisikia furaha Rais Samia anaendesha nchi yetu na sisi wanawake tusishangae ipo mwaka na sisi tutakuja kupambana na kazi ngumu tunafanya,” alisema Halima.