AFISA Mfawidhi wa Shirika la
Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua
kulia akiwaonyesha wavuvi wa namna ya
kuvaa vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini wakati alipokwenda
akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na
wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga mkoani Tanga kutoa elimu ya umuhimu wa usalama
na utunzaji wa mazingira
AFISA Mfawidhi wa Shirika la
Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akisisitiza jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na
wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga
AFISA Mfawidhi wa Shirika la
Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua
kulia akizungumza jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa
vyombo, manahodha na
wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akifuatilia kwa umakini maswali kutoka kwa wavuvi,wamiliki wa vyombo |
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la TASAC Martha Kalvin akieleza jambo kwa wavuvi kuhusu umuhimu wa usalama wawapo kwenye shughuli zao |
Sehemu ya wavuvi,wamiliki wa vyombo na manahodha wakimsikiliza Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua elimu ya umuhimu wa usalama
na utunzaji wa mazingira.
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesisitiza
umuhimu wa wavuvi kuzingatia usalama ikiwemo kuwataka kuacha kufanya
kazi kwa mazoea wanapokuwa katika shughuli za Uvuvi wawapo majini ili
kuwaepusha na vifo,majeruhi na kupoteza mali.
Huku wakisisitiziwa umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea
wanapokuwa majini ili viweze kuwasaidia kuepukana na ajali ambazo
wanaweza kukumbana nazo.
Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la
Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua
wakati na akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na
wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga na Mwalo wa Sahare
Jijini Tanga mkoani Tanga walipokwenda kutoa elimu ya umuhimu wa usalama
na utunzaji wa mazingira.
Alisema kwamba ni muhimu kwao kuweza kuhakikisha
wanazingatia usalama wakati wanapokwenda kufanya shughuli zao kwani hilo
litawaepusha na majanga ambayo wanaweza kukutana nayo na kupelekea
kupata majeraha au kupoteza maisha na mali.
“Serikali imeona hilo ni jambo la msingi sana na ndio maana
tumeona leo tuje hapa Monga Vyeru kuwapa elimu hii ya usalama na
utunzaji wa mazingira hususani mnapokuwa kwenye shughuli zenu hili ni
jambo hilo lakini pia kuhakikisha mnakuwa na vifaa vya uokozi”Alisema
“Kwani tunatambua kwamba pia wavuvi wana familia hivyo
elimu hii itaweza kuwasaidia kupunguza ajali,kuondoa vifo na kupunguza
majeruhi na kuacha familia kuwa tegemezi”Alisema
Afisa Mfawidhi huyo alisema shughuli za usalama sio jambo
la mtu mmoja bali ni watu wote hivyo lazima wahakikisha wanazingitia
sheria za usalama ikiwemo kuvaa majaketi ya kujiokolea “life jacket” ili
yaweze kuwasaidia pindi wanapokumbana na dhoruba baharini waweze
kujiokoa.
“Lakini pia kuhakikisha tunakuwa tunazingatia usalama
tuwapo majini moto unawaka kutokana na mafuta hauwezi kuuzima na maji ni
lazima uhakikisha unatumia mchanga au poda maalumu “Alisema
Hata hivyo alisema ni muhimu na vizuri kwa wenye vyombo
vinavyotumika kwa ajili ya shughuli za uvuvi wanakuwa na watu wenye
ujuzi na kufanya kazi za majini ikiwemo wajibu wa mmiliki kutii sheria
bila shuruti kuhakikisha usalama wake.
Hata hivyo Afisa Mfawidhi huyo aliwataka kuhakikisha kabla
hawajaingia majini kuendelea na shughuli zao lazima wawe na cheti kutoka
kwenye Shirika hilo ambavyo vinawaruhusu kufanya kazi majini.
“Lakini suala jingine sheria imemuelekeza Afisa Uvuvi
asipope leseni ya uvuvi mpaka awe amepata cheti cha Shirika la TASAC cha
kuruhusiwa kufanya kazi majini ”Alisema