Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo CWT, Stella Kiyabo,akizungumza wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Mhadhiri na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Bern, Idara ya Uchumi na Utafiti nchini Uswisi, Dk.Konstantin Büchel,akiwasilisha matokeo ya tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Helvetas nchini, Annet Witteveen,akizungumzia jinsi walivyoamua kuingia kwenye mradi huo kuungana na CWT baada ya kuona kuna uhitaji wa kuendeleza elimu nchini.
Mbunge wa Urambo (CCM) Magreth Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya ushauri wa Mradi wa SITT,akizungumza kwenye Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu CWT Maganga Japhet ,akizungumza wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo, Mwalimu Diana Zakaria kutoka Shule ya Msingi Ololieni Mkoa wa Arusha,akielezea mradi huo ulivyowajengea uwezo wa kufundisha wanafunzi wengi wanaokuwa kwenye chumba kimoja kwa kuwaweka kwenye makundi mbalimbali na kufundisha zaidi ya mada moja.
Meneja Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) Donatian Marusu,akielezea mradi huo ulivyosaidia ufaulu kweye Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Mdhibiti ubora wa Shule za Wilaya ,Robert Assey,akielezea mradi unavyosaidia wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Afisa Elimu Kondoa Mjini Yovin Mtawa,akitoa ushuhuda wa mradi SITT wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Katibu wa CWT Mkoa wa Tabora Digna Nyaki,akichangia mada wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
Mratibu Elimu TAMISEMI Riaz Abbeid,,akizungumza wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Warsha ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
PICHA ya pamoja mara baada ya Kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji Elimu uitwao Inclussive School-based In-service Teacher Training (SITT) unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas jijini Dodoma.
………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MATOKEO ya tathmini ya Mpango wa uboreshaji elimu kupitia mafunzo ya ualimu kazini (SITT) uliotelekezwa kwenye shule 408 za msingi nchini yameonesha kuongezeka kwa ufaulu wa alama za juu kwa asilimia 30.
Kutokana na matokeo hayo, Chama cha Walimu nchini(CWT) kimetoa wito kwa serikali kutoa mafunzo hayo ili kuwa na walimu mahiri na wabunifu nchini.
Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo CWT, Stella Kiyabo, ameyasema hayo leo jijini Dodoma kwenye kikao kazi cha kupokea taarifa ya tathmini ya mradi huo unaofadhiliwa na CWT kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas.
Amesema mradi huo unafundisha walimu mbinu rahisi za kufundishia masomo ya Hisabati, Kiingereza, Sayansi na unajihusisha na masuala ya afya na mazingira.
“Tumetaka wafanye kazi zao kwa urahisi bila kuogopa mada yeyote kwa madai kuwa ni ngumu, CWT inaionesha serikali umuhimu kuwa na mafunzo kazini kwa walimu,”amesema.
Awali akiwasilisha matokeo ya tathmini hiyo, Mhadhiri na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Bern, Idara ya Uchumi na Utafiti nchini Uswisi, Dk.Konstantin Büchel, amesema SITT imeongeza ufaulu wa alama za juu kwa asilimia 30 huku kufeli kukipungua kwa asilimia 10.
Amesema idara hiyo hufanya utafiti wa masuala ya maendeleo na elimu kwenye nchi mbalimbali ambapo kupitia Shirika la Helvetas wamefanya tathmini ya mradi wa SITT.
“Tuliamua kufanya utafiti ili kuona matokeo ya mradi huu katika shule mbalimbali, tulishirikiana na Helvetas Tanzania katika kufanya tathmini kwenye Wilaya za Mbulu, Karatu, Mbulu Mji na Siha ambapo tulishirikisha walimu, wanafunzi, viongozi ambapo wameonesha kufurahia mradi na wapo tayari kuubeba na kuendeleza zaidi kwa ajili ya manufaa ya wanafunzi na walimu,”amesema.
Amesema katika tathmini waliyowafanya wamegundua mradi unaleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji kutokana na walimu kushirikiana, kuwa huru kufundisha na wanawapa wanafunzi nafasi kubwa kama chanzo cha maarifa.
“Tumeona ushirikishaji huo wa wanafunzi shule za mradi zimefanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na la nne, na tumegundua ongezeko la alama za juu yaani A na B zimeongezeka katika shule za mradi kwa asilimia 30 na kufeli kumekupungua kwa asilimia 10, hivyo mradi unaonesha kuleta tija ikilinganishwa na maeneo mengine,”amesema.
Naye, Meneja Mradi huo, Donatian Marusu, amesema mradi huo umefikia shule 408 na walimu 892 kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
“Pia kupitia vyuo vya ualimu tumefikia vyuo 12, tumetoa mafunzo juu ya mbinu shirikishi za ujifunzaji, vitendo na ubunifu wa zana zinazopatikana kwenye mazingira yao, hivyo kupitia mpango wa SITT tumeona matokeo mazuri ni mradi unaofaa tunaomba wadau washirikiane na Helvetas kupanua mradi na kufikia maeneo mengine,”amesema.
Mkurugenzi wa Shirika la Helvetas nchini, Annet Witteveen, amesema waliamua kuingia kwenye mradi huo kuungana na CWT baada ya kuona kuna uhitaji wa kuendeleza elimu nchini.
Amesema kuna haja ya kupeleka mradi huo kwenye mikoa mingine ya Lindi, Geita, Mtwara na Morogoro ili kuwahakikisha wananchi wanapata mbinu mbalimbali za ufundishaji.
Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo, Mwalimu Diana Zakaria kutoka Shule ya Msingi Ololieni Mkoa wa Arusha, amesema mradi huo umewajengea uwezo wa kufundisha wanafunzi wengi wanaokuwa kwenye chumba kimoja kwa kuwaweka kwenye makundi mbalimbali na kufundisha zaidi ya mada moja.
“Mradi wa SITT unamfanya mwalimu kujishusha kuwa sawa na wanafunzi ili kutambua matatizo mbalimbali ya wanafunzi na kuzitatua hii imesaidia kuongeza ufaulu,”amesema.
Mwalimu huyo amesema mafunzo hayo yamemsaidia kufundisha wanafunzi wa kike namna ya kutengeneza taulo za kike za asili hali ambayo imesaidia kuongeza mahudhurio kwa wanafunzi.
Ametoa wito kupanua wigo wa mradi huo ili kwenda mikoa yote nchini kwa kuwa mbinu na elimu ya hedhi ni muhimu ili kuongeza ufaulu na kuwa na wanafunzi mahiri.