MWENYEKITI wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhe.Adam Kimbisa,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhe.Pamela Maasay,akifafanua jambo zaidi kwa waandishi wa habari kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhandisi Mohamed Mnyaa,akizungumzia faida za wananchi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)Mhe.Maryam Ussi Yahya ,akiwahimiza zaidi wananchi kuchangamkia fursa hiyo pamoja na program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhe.Josephine Lemoyan akijibu masawali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mhe.Happiness Lugiko akieleza umuhimu wa kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
…………………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MWENYEKITI wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Adam Kimbisa,amewataka wananchi wa Afrika Mashariki kuchangamkia fursa zinazotokana na mtangamano wa Jumuiya, Bunge la Afrika Mashariki ambalo limeandaa mpango wa kutoa elimu kwa umma kushiriki kwenye utekelezaji wa hatua za soko la pamoja.
Nchi zinazounda Jumuiya wanachama ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burudi, Sudani kusini na Kongo ambayo imemaliza mchakato wa kujiunga hivi karibuni
Mhe. Kimbisa,ameyasema hayo ijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu program ya bunge la Afrika Mashariki ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kimbisa,amesema kuwa lengo kubwa ni kuhamasisha wadau washiriki kwenye utekelezaji wa hatua ya soko la pamoja la Afrika Mashariki.
“Mpango huu unataekelezwa katika nchi zote wanachama kuanzia Aprili 3 hadi 8 mwaka huu”
“Fursa zinahitaji watu wazichangamkie ili ziweze kuwaletea matunda watanzania tunapaswa kuzichangamkia fursa hizo Kwa kushindana na raia wa nchi nyingine wanachama ili tuweze kunufaika na mtangamano wetu na tafiti zinaonyesha kuwa moja ya vikwazo vinavyosababisha wanachama wengi washindwe kuzichangamkia fursa ni kutokuwa na uelewa wa kutosha,”amesema
Aidha amesema kuwa kwa upande wa Tanzania mpango huo unatekelezwa na wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki na katika miji ya Dodoma,Dar es Salaam na Zanzibar.
“Shughuli zinazaofanyika ni pamoja na kuonana na watendaji wa Wizara mbalimbali ili kuona utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kuhusu soko la pamoja, kukutana na waandishi wa habari, kushiriki vipindi vya redio na televisheni na kuonana na wadau mbalimbali.
Pia Kimbisa amesema kuwa Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajia kukutana kabla ya mwisho wa mwaka huu kutangaza kuongezeka kwa muda wa kuanza kutumika sarafu moja kwa nchi zote za Jumuiya.
“Majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha yalikamilika mwaka 2013 ambapo nchi wanachama zilikubaliana kuwa na kipindi Cha maandalizi Cha miaka 10 kuanzai mwaka 2014 na inatarajia kukamilika ifikapo 2024 na BARAZA la Mawaziri litakuta hivi karibuni kwàajili ya kuongeza muda kwasababu bado mchakato haujafika kwenye hatua ambayo kufikia mwaka kesho kutwa itakuwa imekamilika,”amesema
Kimbisa amesema bunge la Afrika Mashariki limetunga sheria mbili za kuanzisha taasisi za Jumuiya zitakazosimamia mchakato wa umoja wa fedha na pia inaendelea na miswada mingine inayolenga kuanzisha taasisi zitakazosimamia utekelezaji wa umoja wa fedha
Kwa upande wake Mbunge wa bunge hilo Mhe.Maryam Ussy Yahya ameswma kuwa katika Jumuiya hiyo wamependekeza jina la sarafu hiyo itakayotumika na nchi za umoja wa nchi za Afrika msahariki iitwe shilingi ya Afrika Mashariki.
Pia amewataka watanzania kuendelea kuchangamkia fursa ya Soko la Afrika Mashariki ambapo hadi Sasa idadi imefikia watu milioni 270 hivyo ni uthibitisho tosha kuwa Kuna fursa za kutosha.
Tanzania inawakilishwa na Wabunge tisa katika bunge la Afrika Mashariki ambao ni Adam Kimbisa, Dk.Ngwaru Maghembe, Maryam Ussi Yahya, Dk. Abdullah Hasnuu, Josephine Sebastian Lemoyan na Fancy Nkuhi