Na. Asila Twaha, TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt. Grace Magembe amewataka Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) kushirikiana na Wakurugenzi, kujua kero za walimu na kuweza kuzifanyia kazi.
Dkt. Grace amesema hayo tarehe 6 Aprili, 2022 Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha mafunzo ya wajumbe wa Kamati ya Tume ya Utumishi wa Walimu wa Wilaya, Kanda ya Kaskazini na Kusini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo ili kuweza kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mafunzo mliyoyapata yakawe ni muongozo mzuri wa kuweza kutekeleza yale mlioyoelekezwa kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu lakini pia msisahau busara na hekima katika utekelezaji wa maamuzi Dkt. Grace amesema, Serikali inatambua nafasi kubwa ya Sekta ya elimu sababu ni watu mnaogusa maisha ya watu moja kwa moja, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema, ataendelea kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia nitoe wito endeleeni kufanya kazi kwa kufuata miiko ya taaluma yenu.
“Tume ya Utumishi wa Walimu kashirikianeni na Wakurugenzi, Maafisa Utumishi ili muwasaidie walimu kwenye kutenda haki mwalimu anayestahili kupewa haki yake apewe haki ya mtu haizulumiwi” Dkt. Grace
Kwa upande wa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Paulina Nkwama ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia amesema, TSC itaendelea kusimamia walimu kwa kufuata Sheria,Taratibu wa upatikanaji wa haki na pale penye ukiukwaji wa maadili ametoa wito kwa walimu kuendelea kufanya kazi kwa kufuata Sheria ya maadili ya Utumishi wa walimu sababu Taifa linawategemea.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Profesa Willy Komba ameishukuru Serikali kwa kuona TSC ni chombo kinachosimamia na kutenda haki ameiomba kuendelea kuiamini Tume hiyo na pale inapoonekana mwalimu amefanya makosa na ikigundulikana hana hatia haki itendeke.
Pia Dkt. Grace ametoa wito kwa walimu hao wakaendelee kuwa walimu wazuri katika kuwaelimisha wananchi katika uandikishaji wa Sensa na kuwaambia walimu hao suala la kuhesabiwa ni moja ya njia ya kuleta mendeleo ya elimu amesema, mazingira mazuri ya walimu husaidia kuleta elimu iliyobora na kupatikana wataalamu.