Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjia akijadiliana jambo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya nchi hizo mbili waliokuwa wakijadili namna zitakavyoshirikiana hususani katika sekta ya sheria na utoaji haki.Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akizungmza na waandishi wa habari kuelezea namna China na Tanzania zitakavyokuwa zikishirikiana hususani katika sekta ya sheria na utoaji haki. Pembeni yake ni balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akifuatilia.
********************
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania na kujadili kwa pamoja namna ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya sheria na utoaji wa haki.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Aprili 7, 2022, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Waziri Ndumbalo amesema kwenye mjadala huo Serikali ya Tanzania imejifunza namna mifumo ya utoaji wa haki nchini inavyopaswa kufanya kazi.
“Tumejidili mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa nchi zetu kwenye sekta ya sheria na utoaji haki. ” Eneo hili ni muhimu kwa kuhakikisha uchumi amani na utulivu wa nchi vinakwenda vizuri”…..balozi ametueleza jinsi China inavyotumia mifumo ya kisheria kuhakikisha uchumi unakuwa.”
“Tumejaribu kuangalia kwa namna gani sheria na mfumo wa utoaji haki nchini unaweza kusaidia kukuza uchumi na biashara kati ya Tanzania ya china.”Amesema Ndumbaro
Amesema kuwa, Tanzania itajifunza mengi kutoka kwa wataalamu wa masuala ya sheria kutoka nchini China na watakaokuja kutoa elimu zaidi na utoaji haki kwa wakati wataalamu wetu pia kwenda nchini humo kujifunza zaidi.
Aidha amesema ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pia ni muhimu…, tunatakiwa kuwa na ofisi ya DPP katika kila Wilaya, lakini mpaka sasa Tanzania ina upungufu wa Ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kwenye Wilaya 125.
“lakini tumeongea na balozi hapa na tumeanza majadiliano ya namna China inavyoweza kutusaidia kwenye ujenzi huo sambamba na kutoa mafunzo kwa wataalamu watakaokwenda kufanya kazi kwenye ofisi hizo.”
Amesema kuwa hatua hiyo itaondoa msongamano wa kesi pamoja na mahabusu.
“Tunaamini Ofisi hizo zikiwepo tutaongeza kasi ya utoaji haki na kupunguza msongamano wa kesi na malalamiko.”
amesema kuwa Balozi wa China amepokea maombi hayo na kwamba wataalamu kutoka nchi zote mbili watakutana kujadili kwa undani.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema kuwa nchi hizo mbili zimejadili mambo muhimu ya kuhakikisha mifumo ya utoaji haki inaimarika.
“Leo nimefurahi kukutana na Waziri wa Katiba na Sheria tumejidili na tumebadilisha uzoefu wa nchi zetu juu ya mahusiano kisheria na kikatiba”
Amesema kuwa nchi hizo zimekuwa zinaurafiki wa muda mrefu na kwamba furaha ya China ni kuona Tanzania yenye mifumo mizuri Hususan ya kisheria.